Machapisho

NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE

Picha
Na,PATRICK SANGA Mithali 14: 1 ‘Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’ . Mchungaji mmoja rafiki yangu aliniambia asilimia hamsini mpaka sabini ya changamoto au matatizo anayoshughulika nayo mara kwa mara katika kanisa lake ni ya wanandoa. Kwa lugha nyepesi asilimia 50 – 70 ni matatizo yatokanayo au yanayohusiana na ndoa. Binafsi pia kwa upande wangu kupitia nafasi yangu katika mwili wa Kristo, email za wasomaji ninazopata na pia baadhi ya semina za ndoa ambazo nimefanya kuhusu eneo hili nimegundua kwa hakika ndoa nyingi za wana wa Mungu zina shida na wao hawajajua kwamba vita hii inatoka kwa Shetani, maana anajua ndoa zikitengamaa ni faida kwa ufalme wa Mungu na ni uharibifu kwenye ufalme wake wa giza. Naam anapigana usiku na mchana ili kuhakikisha ndoa hazitengamai kwa kuleta fujo za kila aina. Kila siku katika ndoa kuna changamoto zinazaliwa mpaka imefika mahala baadhi ya wanandoa wanawaza kwa nini...

AWAMU YA TATU YA MIKOPO ELIMU YA JUU 2017/2018

WANAFUNZI 7,901 WAPANGIWA MIKOPO KATIKA AWAMU YA TATU KWA 2017/2018 Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa orodha ya Awamu ya Tatu ya wanafunzi 7,901 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 29,578. Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo na Awamu ya Pili wanafunzi 11,481. Orodha hiyo ya Awamu ya Tatu inapatikana hapa.   Aidha, orodha hii inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz) na itatumwa kwa vyuo husika. Kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.

MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Picha
Friday, November 3, 2017 Bodi ya mikopo Yawatoa Hofu Wanafunzi Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu nchini (HESLB) imewatoa hofu wanafunzi waliokosa mikopo kwakuwa ipo katika hatua za mwisho kutoa majina ya awamu ya tatu. Kauli hiyo imekuja ikiwa leo   ni siku ya mwisho iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ya kuitaka bodi hiyo kuhakikisha kila mwanafunzi mwenye sifa anapewa mkopo. Akizungumza leo Novemba 3,Meneja Mawasiliano wa bodi hiyo, Omega Ngole amesema agizo hilo linaendelea kutekelezwa na kwamba hadi kufikia kesho  kila mwanafunzi mwenye sifa atapata mkopo. Amesema kwa wale watakaokosa mkopo wanaweza kukata rufaa kupitia bodi hiyo ili kupitia upya taarifa zao. “Maelekezo hayo yote yanatekelezwa na tutakamilisha leo na tutatoa taarifa ya kuhusu utekelezaji wake wiki ijayo,” amesema Katika mwaka wa masomo wa 2017/18 Serikali imetenga bajeti ya...

Job Opportunities at UNHCR Tanzania | AJIRA YAKO

Job Opportunities at UNHCR Tanzania | AJIRA YAKO

KUKUA NA KUIMARIKA ROHONI

“ Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli ” (Luka 1:80)   “ Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima na neema ya Mungu ilikuwa juu yake ” (Luka 2:40) “ kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiogoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu ” (1Petro 2:2) Mtu anahitaji kukua rohoni na kuongezeka nguvu kwa sababu :-   anazaliwa akiwa mchanga rohoni (immature). Mistari hii inatuonesha wazi kwamba mtu anatakiwa kukua sio tu mwili bali na roho yake pia,   kuongeza hekima ndani ya mtu na neema juu yake.   Ili awe na msingi wa mafanikio katika kila Nyanja . “ Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama roho yako ifanikiwavyo ” (3 Yoh 1:2) Kusudi la Mungu ni tufanikiwe katika maeneo yote ya maisha sio tu machache, sio unafanikiwa maswala ya kiuchumi halafu ndoa inakushinda, au unafanikiwa kielimu halafu sehemu ya...

TABIA ZA WATU

   PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YAO Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria hizo ni 1.    Introvant: watu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina hapa kuna makundi mawili 1. Melancolin             2. Fragmetic 2.      extrovants: wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakari za kina katika mambo yao Hapa kuna makundi mawili 1.  Sanguine           2. Colerick Na sasa tuangalie tabia za kila kundi na mienendo yao 1. MELANCOLIN Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo -wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient) -ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi -wanamudu v...

MAMLAKA

VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU . Mwalimu:MWL MWAKASEGE Marko 11: 27-28 ‘’ 27 Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia. Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO? ​ Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5 Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu, 6walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu. 7Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya jambo hili?”’’ ​ Yesu aliulizwa swali hili kuwa ni kwa mamlaka ya nani unafanya jambo hili. Hata wanafuzni wa Yesu pia waliulizwa swali hili. Maana kwa akati ule viongozi wa dini hawakujua kuwa walifanya kwa mamlaka ya nani na ni nani aliwepa mamlaka kwa sababu hawakuwahi ona. Maana wangejua wasingeuliza. Point...