Na,AYOUB JL Uadui ni hali inayokua kwa kasi sana kati ya Ndugu,jamaa na washirikia.Hii ni kwa sababu mwanzilishi anajua siri iliyo katika umoja,ushirika,mshikamano na kuishi pamoja kwa umoja.Maisha ya Ushirika yana nguvu kubwa ya kushinda kila dhoruba inayowakabili washirika.Maandiko yanasemaje juu ya umoja. Yohana 17:22-23 " Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao,ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja,............................................" Mdo 4:32 "Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja,wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alichonacho ni mali yake mwenyewe,bali walikuwa na vitu vyote shirika. Maandiko yanaonesha kuwa Yesu anatamani kuona wanadamu wakiwa katika umoja kama wao walivyo na umoja na Mungu(Yohana 17:22-23) .Haipendezi kuishi maisha ya msuguano wala chokochoko ni jukumu lako kutafuta kwa bidii maisha ya Amani (Ebr 12: 14) Ni jambo la kupendeza kukaa pamoja kwa umoja (Zab 133:1).Tendo la ndugu (jamii ye