NGUVU YA KUUSHINDA UADUI
Na,AYOUB JL
Uadui ni hali inayokua kwa kasi sana kati ya Ndugu,jamaa na washirikia.Hii ni kwa sababu mwanzilishi anajua siri iliyo katika umoja,ushirika,mshikamano na kuishi pamoja kwa umoja.Maisha ya Ushirika yana nguvu kubwa ya kushinda kila dhoruba inayowakabili washirika.Maandiko yanasemaje juu ya umoja.
Yohana 17:22-23 " Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao,ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja,............................................" Mdo 4:32 "Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja,wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alichonacho ni mali yake mwenyewe,bali walikuwa na vitu vyote shirika.
- Maandiko yanaonesha kuwa Yesu anatamani kuona wanadamu wakiwa katika umoja kama wao walivyo na umoja na Mungu(Yohana 17:22-23) .Haipendezi kuishi maisha ya msuguano wala chokochoko ni jukumu lako kutafuta kwa bidii maisha ya Amani (Ebr 12: 14)
- Ni jambo la kupendeza kukaa pamoja kwa umoja (Zab 133:1).Tendo la ndugu (jamii yenye mahusiano ) kukaa pamoja linapendeza sana ,tena maandiko yanafananisha na mafuta katika ndevu za Haruni.Ni jukumu lako kutafuta furaha hiyo iliyo katika tendo la kukaa pamoja.Mipasuko siyo jambo la kupendeza,kaeni pamoja.
Tena ukisoma Kol 1:20-22. "na kwa yeye kuvipatanisha vitu vilivyo na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake,.................
Ndugu yangu dawa ya uadui ni Damu ya YESU pekee,Damu hii inakuletea amani na kuwafanya waliotawanyika kuwa karibu kuliko awali,inasababisha uhusiano uliopotea kurejea kuliko awali maana andiko linasema ya kale yamepita sasa yamekuwa mapya.Damu hii inakufanya kuwa mpya.
Kwa nini usiokoke ? Maana bila kuokoka huna mamlaka ya kutumia damu ya Mwanakondoo .Itaendelea........
Maoni