Ruka hadi kwenye maudhui makuu



SOMO.NGUVU YA MAONO KATIKA MAISHA YA MKRISTO

NA:AYOUB JL

UTANGULIZI.
  1. Tangu mwanzo Mungu aliwekeza raslimali nyingi za thamani ndani ya mwanadamu kama vile Ufahamu,Ujuzi,ubunifu,Ugunduzi,busara,vipaji mbalimbali,mamlaka,uhai,chanzo cha Baraka.Mwanzo 1:26-30,2:7.
  2. Mwanadamu anapozaliwa tayari Mungu anakuwa amekamilisha sehemu kubwa ya uumbaji wa mwili,hivyo anapozaliwa huanza kudhihirisha raslimali hizo katika hali ya upekee tofauti na viumbe vingine.
  3. a) Mamlaka ya kumiliki vitu vyote Mwanzo 1:26-30,2:7
  4. b) Kujitambua
  5. c) Chanzo au  chemichemi  au  chimbuko la Baraka –Kumb 8:18
Zaidi sana mwanadamu anapookolewa , Mungu huwekeza vitu vingine vya    thamani katika maisha ya mwanadamu.Vitu hivi humfanya Mwanadamu  afanye zaidi ya uwezo wa kuzaliwa nao (uwezo wa kawaida).Raslimali hizo ni
  1. a) Huduma,karama na vipawa  1 Kor 12:4-11
b )  Mamlaka ya kumshinda shetani  Lk 10:19, 1 sam 17:40-54
  1. c) Ufahamu wa Ki-Mungu-  Yusufu  Mwanzo  41 :37-40, Dan 1 :17-20
d )  Milango ya Baraka za Mungu –Mdo 10:34-35
Swali.Kama Mungu kawekeza raslimali nyingi za thamani kiasi hicho tangu kuumbwa hadi kuokoka.Kwa nini watu maisha  yao  hayadhihirishi kile alichoweka Mungu ndani yao ?
Mithali 29:18 “Mahali pasipo na  maono, watu huangamia,  bali ana heri mtu yule aishikaye sheria”.Where there is no vision,the people perish…………..AMPLIFIED BIBLE).
Nini maana ya maono ?
  • Ni picha halisi ya hatima itarajiwayo(the true image of the future).
  • Ni ndoto ya mambo ya mbele
  • Ni unabii wa maisha mapya toka kwa Mungu -Yer 1:4-12,Kut 3 :1-4
  • Ni zawadi ambazo Mungu aliahidi kutimiza kwa kanisa –Yoel 2 :28
  • Ni njia ambayo hutangulia jambo kabla ya kudhihirika na kutendeka –Amo 3:7
  • Ni siri ya Bwana -Amo 8:11-12,1 Sam 3:1
  • Ni sura tarajiwa ya maisha ya mbele (Mwanzo 13:14-18,Mith 23:7)” Maana aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo
  • Ni njia mojawapo ya mawasaliano kati yetu na Mungu Mdo 9:10-
SABABU ZA KUWEPO MAONO
  • Humfanya mtu asichukuliwe na upepo wa kila aina. Mwanadamu asiye na maono hujikuta ametumbukia mahali asipopataka –Hos 7:9
  • Humpatia mtu tahadhari ya hatari iliyo mbele Mwa 15:1
  • Ili tuweze kumwona Mungu mbingu zinapofunguka Eze 1:1
  • Ili tuweze kumpatia sifa Mungu Dan 2:19-20
  • Humwelekeza mtu anakokwenda(it  gives us our live direction).Mtu asiye na maono ni sawa na kipofu asiyejua anakokwenda maana andiko linasema Pasipo maono njia yote ni giza kuu.Amo  8;11-12,1 Sam 3:1,Math 15:14,Mdo 9:10
  • Maono hupanua wigo wa fikra zetu,bila maono watu wanakuwa na fikra finyu(maono ya kuku ),badala ya maono ya tai (chicken vision instead of eagles vision)
  • Maono yanamwezesha mtu kuziona fursa na mipango mikubwa ya Mungu iliyo mbele yake( Yer 29:11, Yoh 15:13-15,Lk 1:22)
  • Maono humfanya mtu avumilie apitapo katika magumu.Wakati mwingine unaweza kupita katika wakati mgumu na vipingamizi vingi lakini kitu kinachoweza kukufanya uendelelee mbele,uendelee kupambana ni ramani uliyonayo(MAONO ULIYONAYO).Mtu anayesimamia maono yake hata wakati mgumu uwezo wa Ki-Mungu(ulio ndani yake) wa kuvuka hujitokeza.Na mtu akishavuka anashangaa na anapofikiria hujiuliza maradufu eehe niliwezaje kupita hapo !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!(Kut 19:4-5,Mwanzo 41:41-)
CHANGAMOTO ZA KUFIKIA MAONO
Wakati ukiwa katika safari ya hatima ya maisha yako ,kuna kila namna mbalimbali zinazoweza kuinuka juu yako lengo lake ni kukufanya usifike mwisho /usipate mwonekano halisi wa picha/dira/ramani ya kile ulichoona(1sam 17:1-).Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na
  • Hofu/mashaka kut 4:1-
  • Kukatishwa tamaa (kuvunjwa moyo) Yosh 1:1-,Kumb 31:6
  • Uvivu-kutochukua hatua dhidi ya maono –Hag 2:4,Hab 2:1,1:1
  • Vishawishi –Luka 8:14
  • Kukosa subira/ Uvumilivu- Yosh 39:1-23,Zab 105:17-21(19)
  • Changamoto za kiuchumi (umaskini).
NINI KIFANYIKE KAMA HUNA MAONO ?
  • Omba Mungu –Math 7:7
  • Soma neno la Mungu na kulifanyia kazi
  • Ishi maisha matakatifu –Yoel 2;28
  • Ishi maisha yanayoongozwa na malengo(Purpose driven life)
  • Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kuijua siri hii,omba utakaso kwa makosa uliyofanya hadi sasa kisha Mtukuze yeye.Nina amini yeye ni mwaminifu atamimina upako na kuzifufua raslimali ziliwekwa ndani mwako.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO