CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) jana tarehe 18.02.2016 lilitangaza matokeo ya Mitihani ya kidato cha NNE na kuleta taharuki kwa wadau mbalimbali kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kushindwa kufaulu kwa kupata ufaulu wa chini.
Nimesikia watu wengi wakieleza kuwa wanafunzi wengi walikuwa na ufaulu usiostahili wakati walipofanya Mitihani ya kuingia kidato cha tatu mwaka 2013 na hivyo kujikuta wakishindwa kumudu masomo ya kidato cha tatu 2014 na hivyo kutahiniwa kwao kidato cha Nne kulikuwa hakustahili kwa kuwa hawakuweza kumudu hata masomo ya kidato cha kwanza na pili ili kuendelea na kidato cha tatu.
Aidha yapo maswali mengi yanayoulizwa kuhusiana na matokeo hayo.Nini kifanyike?
  1.     Mitihani ya kidato cha pili iheshimiwe ili kupata wanafunzi wenye kumudu stadi mbalimbali katika nyanja za uchumi,siasa na jamii.
  2. Masuala ya Kitaaluma yaendeshwe kitaalamu pasipo kubadilishwa pasipo tija kama ilivyokuwa kutoka Division mara GPA.
  3. Suala la michepuo kwa wanafunzi liwekewe kanuni na miongozo kuliko kuendeshwa kutegemea shule.Mfano mwanafunzi asome Sayansi kutegemea ufaulu wake katika Mitihani ya kidato cha pili ili Mitihani hiyo iitwe 'Placement examinations" na wapangwe mara baada ya matokeo kutoka.
  4. Jamii ijenge utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao kila ngazi ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuchukua hatua stahiki kwa wakati mwafaka bila kuchelewa.
  5. Wanafunzi waliofeli wasiachwe bali watafutiwe njia mbadala ya kuwasaidia kwa kuwa ni wengi wakilinganishwa na waliofaulu.
  6. Wanafunzi walioko shuleni wasome kwa malengo na kwa bidii wakijua kuwa Malengo na Jitihada huzaa matokeo mazuri.
         Na.Ayoub JL

Maoni

kweli matokeo yameporomoka sana,sababu kuu ni zifuatazo 1,walimu kutokuwa na wito wa kufundisha kwa kutofuata weredi wa TAALUMA zao/professionalism.2,mtihani drs LA saba kutokidhi kiwango kinachotakiwa kwa kutumia upimaji mbovu hasa kwa somo la hesabu ambapo mwanafunzi hulazimika kuchagua majawabu badala ya kukokotoa na kupata jawabu sahihi hii inachangia kuwa na majibu ya kubuni/guessing answers na kupelekea kushinda watoto wengi wasio na ubora(quantitativeness &not qualitativeness)mfumo wa zamani urudishwe ili mwanafunzi afaulu kwa uhalisia na si kwa nadharia km ilivyo sasa.3,wanasiasa wanaingilia sekta ya elimu kwa utashi wa kisiasa kwa mf.kulazimisha standardization ili kuwa na uwingi wa walioshinda na sio waliofaulu.4,kukumbatia utandawazi wenye matokeo hasi ambao unaondoa maadili ya kitanzania hasa kwa wanafunzi .5,walimu wa serikali kutopewa motisha za kufundishia/teaching allowances 6,upungufu wa vifaa vya kufundishia hasa kwa masomo ya sayansi .7,mrundikano wa wanafunzi darasani has a shule za SERIKALI hivyo kuchangia usomaji hafifu kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.8,uhaba wa walimu hasa wa masomo ya sayansi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO