SOMO : WAJIBU WA KUTHIBITI ULIMI


MCH. TUMSIFU KASSA
 
YAK  3: 1-12
Ulimi una kazi kubwa sana.Baadhi ya kazi za ulimi kwa binadamu ni kutoa sifa na laana.Ulimi wa mtu aliyeokoka una kai kubwa kuliko wa mtu wa kawaida.
Tutumie ulimi kwa uangalifu mkubwa sana.
Baadhi ya watumishi wa Mungu waliotangulia walishindwa kuthibiti ndimi zao kama vile,Nuhu,Musa, Samson, Eliya n.k.Ndiyo maana maandiko yanasema kuwa aliye Mkamilifu pekee ni Mungu tu.(Mhubiri 7:20)
Mungu anatafuta watu wanaothibiti ulimi ili wamtumikie.Mith 10: 19-20,21.
Mungu anakusudia ulimi uwe kama fedha teule.
Kwa kutumia ulimi tunahubiri injili,kuombea wagonwa,kufukuza mapepo,kumsifu Mungu.
Watu wengi sana katika ndimi zao wametamka kutamani nguvu Za Mungu lakini hjawako tayari kutafuta Mungu mwenye nguvu.Kanuni za kufundisha zinataka kila anayefundisha kwanza awe amejifunza au amebadilishwa na neon analofundisha ( Math 22: 15-16).
Mafundisho mengi yanasisitiza juu ya mafanikio hayamzungumzii Mungu. Sikiliza mtu wa Mungu,MAFANIKIO NI KITU KIDOGO KWA MTU  ALIYEOKOKA” ni sawa na RUZUKU.
MAMBO MATATU JUU YA ULIMI
     i.        ULIMI NI CHANZO KIKUU CHA DHAMBI.
Dhambi nyingi husababishwa na ulimi.Ni chanzo kikubwa cha dhambi.
    ii.        ULIMI NI CHANZO KIKUBWA CHA KUPOTEZA NGUVU ZA MUNGU.
a)      MUSA
Hes 11: 1-12 Wakati Mungu anamwita alisema kuwa ulimi wake ni mzito,lakini baadae Musa huyo huyo anasema hawezi kuwavumilia wana Israeli kwa kuwa hakuwatungia mimba mbele za Mungu.
Mtu wa Mungu,Mungu akikuamini katika utumishi usitumie ulimi vibaya kwa kumkufuru au kusema maneno mabaya.Badala tafuta kujua wewe umeitwa kama nani ?
b)      PETRO MTUME  ( Math 26: 69-75)
c)      SAMSONI  ( Waamuzi 13: 1-5 )
Ni vizuri kujua makusudi ya Mungu kukupa mtoto.
Tambua uliye naye ana kitu gani ?
TUANGALIE JINSI MUNGU ALIVYOMTUMIA SAMSONI,
Waamuzi 14 : 5-6  Samsoni alimchana simba bila silaha.
WATU WENGI WANATAKA KUWA NA BARAKA ZA MUNGU LAKINI HAWATAKI MUNGU MWENYE BARAKA
Waamuzi 15 : 4-5 Samsoni anaunganisha mikia ya mbweha na kuunguza masuke ya ngano
Mungu atakupa moto wa kuteketeza matita ya Shetani
Mark 16 :16
 Mamlaka ya Mungu ni muhimu sana kwa mtu wa Mungu (Waamuzi 15 : 14 -15 )
Ukiwa na nguvu za Mungu utaangusha maadui wengi.
MATUMIZI MABAYA YA ULIMI WA SAMSON
Waamuzi 16 : 4-6, 13 – 14, 15-  21.
Watu wengi wanaujuaji usio na maana .Mtu aliyeokoka anatakiwa kuwa na ujuaji huu Rum 16 : 19  Kila mtu amesikia juu ya utii wenu na nimekuwa na furaha kwa ajili yenu. Lakini napenda muwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu. Biblia Takatifu )
Ujuaji uwe katika kutafuta hekima na kutafuta mambo mema.Uwe mjinga katika mabaya.
HATUA ZA KUUTHIBITI ULIMI
i)             Fanya maamuzi ya kuutumia ulimi wako vizuri Zab 34 : 13,:39 1-2
Tunza ulimi wako vizuri.
Ni uamuzi wako kuutumia ulimi vizuri au vibaya.Maamuzi yako mikononi mwako,ukiamua inawezekana.
ii)                  Mwombe Mungu aponye ulimi wako Zab 34 : 11-13,1 Pet 3: 10 ,Zab 120 : 2
Wokovu ni mabadiliko yasiyokoma.Unaweza ukawa unatumika lakini ukawa na tatizo katika ulimi wako mwombe Mungu akufinyange.Msogelee Mungu anaweza kuutengeneza ulimi wako na ukawa Mtumishi mwema.
iii)                Tamani Neno la Mungu likutengeneze Isa 6: 1-7 ,5-7 kumbuka Isaya alikuwa NABII mkubwa lakini ulimi wake ulikuwa unaongea maovu .Anakumbuka kwamba Mungu pekee anaweza kuchoma midomo midomo yake na kuwa bora.
Ndugu mwombe Mungu achome ulimi wako.Ukichomwa na kaa la Bwana utasikia sauti ya Mungu.
iv)                Endelea  kutamani  kutakaswa na NENO LA BWANA.Zab 119 : 9,105.
Tamani kumulikiwa na NENO LA MUNGU
MUNGU AWABARIKI
MCH.TUMSIFU KASSA
FPCT MWAHURI –KISESA
10.07.2016


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO