ROHO MTAKATIFU NI UFUNGUO WA MAMLAKA KWA KANISA
NA,CHARLES SYLIVESTER
FUNGUO YA TANO : ROHO MTAKATIFU
Rejea
somo lililopita “FUNGUO ZA MAMLAKA KWA MKRISTO”
- Jina la Yesu Kristo
- Damu ya Yesu Kristo
- Roho Mtakatifu
- Neno la Mungu
- Maombi .
- Roho ni kila kitu siyo msaidizi kwa maana kwamba hana mamlaka
- Roho ni mtu kwa sababu anaishi anatumia.
- Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana kwa kanisa.
- Mwambie Roho Mtakatifu akujaze nguvu mpya.Usikubali ukaondoka bila kupokea nguvu za Roho Mtakatifu.
- Roho Mtakatifu ni ufunguo milango na malango.Ni zaidi ya nguvu za kawaida.Mkristo aliye na nguvu za Roho Mtakatifu anakwenda kwa viwango tofauti na mtu wa kawaida
- Roho Mtakatifu ili ashuke kwako lazima uwe katika hali ya maombi.
- Roho Mtakatifu akithaminiwa kila mahali anakuwa pamoja nasi kwa kila jambo na kila mahali.
Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana katika maisha yako.
KAZI ZAKE
1. Hutuongoza kwenye
kweli yote(Yoh 16:13).Kama unataka kuwa
mkweli lazima uwe na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni mzuri anakujulisha kwa
habari ya mambo yajayo.Mtu wa Mungu anatakiwa kutengeneza mahusiano na Roho
Mtakatifu.Ukiwa na mahusiano atakujuza habari ya kweli zinazokujia mbeleni.Si wa kawaida katika maisha yetu.
2. Hutuongoza katika
maombi.Maombi yenye nguvu
huongozwa na Roho Mtakatifu “LK 4:1..na Yesu,hali amejaa Roho Mtakatifu,alirudi
kutoka Yordani,akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani”.Roho Mtakatifu
ndiye hukutofautisha na watu wengine.Kanisa bila Roho Mtakatifu ni kusanyiko la
dini.Kila mtu anayetaka kufanikiwa katika maombi anapaswa kuomba uongozi wa Roho
Mtakatifu
3. Hutufanya kuwa
mashahidi wa Yesu Mdo 1:8.”Lakini mtapokea nguvu,akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu,nanyi
mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote,na Samaria
,na hata mwisho wa nchi”.Tukimshika Roho
Mtakatifu hatutakuwa yatima kwa kuwa yeye atatufanya kushuhudia matendo makuu ya
Mungu kwetu.Wakristo wenye nguvu ya Roho Mtakatifu wanamtangaza na kumtetea
Yesu
4. Hutufanya kuwa washirika
wake (Partners of Holy Spirit)2cor 13:14.Huyu
ni wa karibu yako kuliko mwingine.Anataka kuona mahusiano yetu yanakuwa
mahusiano yetu yana imarika. Jifunze kumwalika Roho Mtakatifu hawezi
kukukatisha tama,ni msiri,hatoi vitu vyako hadharani.Ni mwaminifu anayeweza
kukusaidia kukuombea.Rum 8:26.Kadhalika
Roho naye hutusaidia udhaifu wetu,kwa maana hatujui……….Jitahidi kujenga
ushirika na Roho Mtakatifu.Unapopata jaribu siyo la marafiki au jamaa zako bali
si lako unahitaji mshirika wa karibu,mke au mme siyo lako.Kumbuka ili imani
yako ikue inahitaji jaribu.
Usimwumize Roho Mtakatifu,jitahidi kuimarisha mahusia
yako nay eye.Boresha mahusiano 2Cor 13:
14
5. Hutuombea kwa kuugua
Rum 8: 26 unapopita katika maumivu Roho Mtakatifu huchukua udhaifu
wako,maumivu anayabeba kama yake ili mwana wa Mungu apate nguvu.Tunamhitaji Roho
Mtakatifu ili tupate nguvu za kumshuhudia kwa watu wengine.Math 27:50 Wakati Yesu
anafufuka makaburi yalitikisika.
Mkristo
a) Tafuta nguvu za Roho Mtakatifu ili akusaidie
b) Tafuta ufahamu kabla ya mafanikio.Mafanikio nimuhimu sana
lakini Roho Mtakatifu ni wa kwanza.Kumbuka Sulemani alivyofanya aliomba hekima
kabla ya kitu kingine.
c) Tafuta Mungu aachilie nguvu zake
d) Tafuta Roho Mtakatifu akupe hekima ili ujue la kufanya
.Yeye atakupa hekima isiyo ya kawaida.
e) Yanayoshindikana kwa wanadamu kwa Roho Mtakatifu yanawezekana.
f) Hakuna adui anayeweza kukupata kama una nguvu za Roho
Mtakatifu.
g) Omba Roho Mtakatifu akujaze kwa ujazo usio wa kikombe
uwe wa Bahari.Omba Mungu akujaze
Somo hili lilifundishwa
katika semina za Pentecoste FPCT KISESA.
MATUKIO KATIKA PICHA
Hakika ROHO MTAKATIFU ni msaidizi na Kiongozi Mkuu. |
Mhubiri katika semina za Roho Mtakatifu.Mwl,Charles Sylvester kutoka Mugumu-Serengeti(MARA) |
MHUBIRI AKIENDESHA MAOMBI |
WAKRISTO WAKINENA KWA LUGHA |
UPAKO WA MAFUTA ROHO MTAKATIFU |
Roho Mtakatifu kwa Wakristo |
Maoni