TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                                    
                                    Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
                                
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
                                    OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
                                
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
“Kwa mshituko na 
masikitiko makubwa nimepokea taarifa za kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa 
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Kanda ya Afrika Kusini Dkt. 
Tonia Kandiero aliyefariki dunia ghafla jana usiku tarehe 28 Juni, 2017 
akiwa ofisini kwake huko Pretoria Afrika Kusini”
Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. 
John Pombe Magufuli aliyoitoa leo tarehe 29 Juni, 2017 Ikulu Jijini Dar 
es Salaam muda mfupi baada ya kupokea taarifa za kifo cha Dkt. Tonia 
Kandiero ambaye kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa
 AfDB katika Ofisi za Kanda ya Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka 2016 
alikuwa Mwakilishi wa AfDB Tanzania.
“Nitamkumbuka Dkt. Tonia Kandiero kama mchapakazi hodari 
aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu, nikiwa Waziri wa 
Ujenzi nimeshirikiana nae kwa karibu kufanikisha utekelezaji wa miradi 
mikubwa ya maendeleo kwa nchi yetu ambayo imefadhiliwa na AfDB, ametoa 
mchango mkubwa kufanikisha ujenzi wa madaraja na barabara za Dodoma – 
Iringa, Dodoma – Babati, Namtumbo – Tunduru – Mtambaswala, Arusha – 
Taveta – Voi na pia alitoa mchango mkubwa katika kufanikisha miradi 
mingine ambayo ipo mbioni kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa barabara ya 
Bagamoyo – Tanga – Mombasa, Mbinga – Mbambabay na Tabora - Katavi”.
Kufuatia kifo cha Dkt. Tonia Kandiero Mhe. Rais Magufuli amemtumia 
salamu za rambirambi Rais wa AfDB Dkt. Akinwumi Adesina, familia ya Dkt.
 Tonia Kandiero, wafanyakazi wote wa AfDB, ndugu, jamaa na marafiki wote
 walioguswa na msiba huu.
Dkt. Magufuli amemuombea marehemu Dkt. Tonia Kandiero apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULUDar es Salaam
29 Juni, 2017
Maoni