NILIMLISHA MUME WA MTU, LIMBWATA LA NYAMA YA BUNDI.
USHUHUDA
WA THEOFLIDA WA YESU :
Nawasalimu kwa jina la YESU,
jina kuu kupita majina yote.
Jina langu ninaitwa Theoflida ,
ni mwanamke mwenye umri wa miaka 38 mkaazi wa Mbezi ya Kimara jijini Dar Es Salaam,
japo kiasili ni mwenyeji wa wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro.
.Nimeamua kuandika waraka huu
kwa madhumuni makuu mawili, kwanza ni kushuhudia MATENDO MAKUU ambayo YESU
AMENITENDEA na pili, ni kuwaasa wanawake wenzangu kutojihusisha kabisa na
masuala ya WAGANGA WA KIENYEJI kwa sababu waganga wa kienyeji ni MAWAKALA WA
KAZI ZA SHETANI HAPA DUNIANI na ni MASHETANI KABISA!...Nitaanza kwa kuelezea
kisa kilicho nipelekea kuingia kichwa kichwa kwenye mikono ya wakala wa
shetani..
Nilikuwa nimepanga chumba kimoja
maeneo ya Tabata Mawenzi huku nikijihusisha na biashara ya genge. Jirani na
nyumba niliyokuwa nimepanga, aliishi mwanaume mmoja na mke wake. Mwanaume huyu
jina lake linaanzia na herufi K hivyo katika maelezo yangu nitakuwa nikimtaja
kwa herufi K.K alikuwa ni mwanaume mwenye mafanikio makubwa katika maisha
mwenye kazi nzuri. Alikuwa na nyumba zaidi ya moja, magari ya kifahari. viwanja
, mashamba, na miradi mbalimbali iliyokuwa ikimlipa vizuri sana.
Kwa ufupi K alikuwa tajiri
mwenye maisha mazuri.K na mke wake wote walikuwa wenyeji wa wilaya ya
Muleba,mkoani Kagera . Ndoa ya K na mkewe ilikuwa na umri wa mwaka mmoja...K na
mke wake waliishi maisha mazuri sana....Kwa sababu ya ugumu wa maisha yangu,
nikajikuta naanza kutamani maisha ya mke wa K.. Nikawa natamani mimi ndo
ningekuwa mke wa K na kufurahia maisha vile mke wa K alivyo kuwa akifurahia.
Nilimuona mke wa K kama mtu mwenye bahati sana na kutamani bahati hiyo iwe
yangu.
Baada ya wazo hili kukomaa
ndani ya nafsi yangu, nikaanza kutafuta njia ya kumteka K kimapenzi na kuchukua
nafasi ya mke wake. Njia pekee niliyo ona inafaa, ni kutumia uchawi.Sasa basi,
kuna rafiki yangu mmoja, anaitwa Pamela. Pamela alikuwa anapenda sana mambo ya
waganga waganga, kwa hivyo alikuwa anawajua waganga wengi. Hata katika biashara
yangu ya genge, alishanipeleka kwa waganga kadhaa kwa ajili ya kupata dawa ya
mvuto wa bishara yangu..Nilipo mfuata Pamela, akaniambia kuna mganga mmoja, ni
mkali sana wa mambo ya mapenzi.. Mi mwenyewe nina mpango wa kumtafuta lakini
najipanga kwanza kwa sababu bei zake ni kubwa.Pamela akasema alimfahamu mganga
huyo alipokuwa katika kijiji cha Mwalusembe, wilayani Mkuranga.. Siku hiyo kuna
fumanizi lilitokea, mwanaume alikuwa anatembea na mke wa mtu, kumbe huyo
mwanamke alikuwa amewekewa tego, huyo mwanaume alipo muingilia mwanamke huyo,
wakawa wamenasana..
Baadae ikatafutwa namba ya simu
ya mume wa mwanamke. Mume alipofika kufumania, akakuta mke wake amenasana na
mgoni wake.. Akaitwa huyo Mganga kwa sababu ndie aliye weka hilo tego,
alipofika eneo la tukio alifanya uganga wake, wale wagoni wakawa wameachana..
Tukio hilo lilivuta watu wengi sana.. Kwa hiyo Pamela anasema, alimjulia mganga
huyu kwenye tukio hilo... Akafanikiwa kutafuta na kupata namba zake.
Pamela akanipa namba za simu za
mganga huyo, nilivyo mpiugia akasema yupo Handeni kikazi ila baada ya siku tatu
atakuwa Bagamoyo ambapo atakaa hapo kwa mwezi mzima aki agua watu wenye
matatizo mbalimbali.Kweli baada ya siku ya tatu, nikaenda hadi Bagamoyo kuonana
na huyo mganga ambaye jina lake tu ni kufuru kubwa kwa Mungu.,. Yeye anajiita
MUNGU WA KABILI ambayo tafsiri yake ni MUNGU WA PILI. Lakini pia nilishangaa
kumuona mganga mwenyewe anaokena bado kijana ambaye sidhani kama ana fikisha
miaka arobaini.
NAANZA KWA KUPIMWA MWILI WANGU
KICHAWI
Mungu wa Kabili akasema kabla,
hajaanza kazi ya ‘kumtengeneza’ K , inabidi aanze kwanza kuuangalia mwili wangu
ili ajue kama ni msafi ama mchafu.Basi nikapewa dawa nimeze, halafu nikaambiwa
Yule kuku mweusi ambaye nilienda nae mwenyewe, nimshike kichwani. Baada ya
hapo, Dokta Mungu wa Kabili akaanza kuongea maneno yake ya kiganga huku akiwa
ameshikilia chungu chenye dawa iliyo katika mfumo wa maji maji..
Alifanya hivyo kwa muda wa kama
dakika kumi na tano hivi. Alipomaliza kufanya uganga wake, akaniambia nimtue
Yule kuku mweusi niliekuwa nimembeba kichwani. Nilipo mtua nikashangaa kumuona
kuku Yule amekufa. Niliogopa sana .Basi Mungu wa Kabili, akaniambia mwili wangu
ni mchafu sana. Roho ya mauti imepandwa kwenye mwili wangu. Hivyo lazima
anisafishe kwanza, kutoa uchafu ulio pandikizwa mwilini wangu kichawi.
Baada ya hapo ndio tutaendelea
na zoezi la kumfanyia ulozi K.Mungu wa Kabili akaniambia niende nyumbani,
nirudi siku inayo fuata jioni ya saa kumi na mbili nikiwa na sarafu 350 za
shilingi mia mbili mbili ambazo jumla yake ni Shilingi Elfu Sabini, mchanga wa
njia panda saba, pamoja na wembe tatu..
NASAFISHWA MWILI WANGU KICHAWI.
Ilipo fika saa sita kamili za
usiku, mimi , Dokta Mungu Wa Kabili pamoja na msaidizi wake, tukaongozona hadi
njia panda. Njia panda hiyo ipo huko huko Bagamoyo porini.. Tulibeba, kigoda,
chungu , vifaa nilivyo kuja navyo ( mchanga, wa njia panda saba, sarafu 350,
pamoja na asali nusu lita ), mawe matatu, mishumaa ya rangi nyekundu, mkaa,
pamoja na dawa nyingine zilizokuwa kwenye vibuyu kama saba hivi.
Tulipofika eneo la njia panda,
Mungu wa Kabili, alizungushia dawa kuzunguka eneo tulipoweka vitu vyetu,
akamuagiza msaidizi wake, awashe mishumaa ambayo idadi yake ilikuwa kumi na
nne, mishumaa hiyo iliwekwa kuzunguka eneo tulilokuwa sisi. Baada ya hapo,
ukawasha moto, kwenye mafiga kisha chungu kikatengwa pale, nikaweka vitu vyangu
vyote nilivyo kuja navyo, na yeye Mungu wa Kabili, akachanganya dawa zake anazo
zijua mwenyewe… Baada ya kama dakika arobaini hivi, zile dawa zikawa zimecheka,
nikapewa kibuyu nikaambiwa nikoge kwa kuchota maji ya kwenye chungu huku chungu
kikiwa kinachemka. Nikafanya kama nilivyo elekezwa huku mganga akiwa anaongea
vitu vyake vya kiganga ambavyo sikuweza kuvielewa.
Nilipomaliza kuoga, mganga
akanichanja karibu mwili mzima, kisha nikapakwa hiyo asali. Baada ya hapo,
tukarejea kilingeni . Mungu wa Kabili akaniambia nipumzike, ikifika saa kumi na
moja alfajiri niamke kwa ajili ya kupikwa. Akasema zoezi la kwanza lilikuwa
kunisafisha na kuniosha kwanza, ambalo limeshakamilika, kinacho fuatia ni
kupikwa.
NAPIKWA KICHAWI…
Ilipofika alfajiri nilidamka,
kama nilivyo agizwa na mganga kwa ajili ya zoezi la kupikwa kichawi..
Nikaelekezwa kuingia katika chumba maalumu ambako kulikuwa na chungu kikubwa.
Ndani ya chungu hicho yaliwekwa maji ya baharini, majani ya mti unaitwa muosha
fedha ama mfedha mfedha, majani ya mkaratusi pamoja na majani ya mti unaitwa
mkuyu, halafu ndani yake zikawekwa sarafu zilizoisha kutumika muda wake, pamoja
na dawa nyingine kama tano hivi ambazo sikuambiwa ni dawa gani…
Baada ya hapo, nikaambiwa
nikatwe nywele zangu, pamoja na kucha zangu. Baada ya kukatwa nywele zangu,
vitu vyote hivyo vikachukuliwa vikafungwa kwenye kitambaa chekundu, ndani ya
kitambaa hicho zikaongezwa dawa nyingine , halafu vikawekwa kwenye chungu kwa
ajili ya kupikwa.Katika chungu hicho pia vikawekwa visu saba, vikiwa
vimesimama. Baada ya kama dakika kumi na tano hivi, mganga akamwambia msaidizi
wake, ‘ hebu ongeza chumvi humo ‘. Nikatarajia kuona itakuwa chumvi ya kawaida
ninayo ijua mimi, ila nikashangaa kuona kinawekwa kipande cha mti..
Baadae nilikuja kugundua kuwa,
katika uganga na uchawi kuna kitu kinaitwa ‘Chumvi ya Kichawi” kazi ya chumvi
ya kichawi ni kuukoleza uchawi ama kukoleza nguvu ya dawa. Mganga aliniambia
vitu vyangu yaani nywele pamoja na kucha vinaniwakilisha mimi, kwa hiyo kupikwa
kwa vitu vyangu kunamaanisha mimi ndio nimepikwa. Baada ya dawa kupikwa,
nikapewa maji yale na kuelekezwa kwenda kuoga. Nikaambiwa nikimaliza kuoga
niende nikapumzike kwenye chumba change hadi nitakapo pewa maelekezo mengine.
NAFANYIWA TAMBIKO LA JUA
Ilipo fika saa sita mchana,
nikapewa dawa Fulani ya kujipaka, halafu nikapelekwa kwenye eneo la juani,
ambalo chini kuna mchanga. Hairuhusiwi kuwa katika eneo hilo ukiwa na viatu.
Baada ya kukaa katika eneo hilo kwa kama dakika arobaini hivi , mganga alianza
kufanya uganga wake pale huku akitamka maneno yake ya kiganga. Baada ya hapo,
akanifuata akanikabidhi kibuyu mkononi na kuniambia nikishike kwa mikono yangu
yote miwili kisha nizungumz nizungumze maneno yafuatayo :“
EWE JUA! MIMI NA WEWE, TU KITU KIMOJA SASA!
WEWE NI MIMI NA MIMI NI WEWE. HAKUNA MTU YOYOTE YULE AWEZAE KUTUTENGANISHA.EWE
JUA!TANGU UANZE KUWEPO, HAUJAWAHI KUISHIA NJIANI.VIVYO HIVYO, MIMI PIA, SITO
ISHIA NJIANI. NITAFANYA MAMBO YANGU YOTE, NITAISHI MIAKA YANGU YOTE KWA KADRI
MWENYEZI MUNGU ALIVYO NIKADIRIA , WALA HAKUNA MTU YOYOTE YULE ATAKAE WEZA
KUNIZUIA, KWA CHOCHOTE KILE NITAKACHO TAKA KUKIFANYA…KAMA WEWE JUA UMEWAHI
KUISHIA NJIANI, BASI MIMI PIA, NITAISHIA NJIANI. NA KAMA KUNA MTU ANAWEZA
KUKUZUIA WEWE JUA, BASI MIMI PIA NAWEZA KUZUILIKA. LAKINI KWA KUWA WEWE JUA
HAUJAWAHI KUISHIA NJIANI, MIMI PIA, SINTOISHIA NJIANI. NA KWA KUWA HAKUNA MTU
YOYOTE ANAYE WEZA KUKUZUIA WEWE JUA, BASI MIMI PIA, HAKUNA MTU YOYOTE ATAKAE WEZA
KUNIZUA…
Niliagizwa kutamka maneno haya
mara arobaini. Kila nilipo maliza kutamka, nilinyweshwa dawa na mganga, kutoka
kwenye kibuyu alicho kuwa nacho… Baada ya zoezi hili kukamilika tulirejea
kilingeni ili lianze zoezi la ‘ kumtengeneza’ K, mume wa mtu mwenye pesa.
NAPEWA DAWA ZA KUMTEGA “K”Tulipo
rudi kilingeni, Mungu wa Kabili akaniambia nimpe majina yangu kamili pamoja na
jina la huyo mwanaume ninae mtaka. Nikafanya kama alivyo niambia. Akayachukua
yale majina, akaandika andika vitu vyake ambavyo sikuvijua vizuri, baada ya
hapo akachukua kioo chake, akawa anatazama kwenye hicho kioo, kisha akachukua
dawa kutoka kwenye kibuyu, akaweka kwenye chungu ambacho ndani yake kulikuwa na
maji…. Baada ya kama dakika kumi na tano hivi, akaniangalia halafu akacheka
sana..
Akaniambia niweke kiganja
changu kwenye kile chungu nikafanya hivyo..Basi akachukua dawa kutoka kwenye
vibuyu vitatu, ambazo alizifunga kwenye vitambaa vitatu tofauti kila kitambaa
na dawa yake, kisha akanipa dawa hizo na kunipa maelekezo yafuatayo : Dawa ya
kwanza, utakunywa na maji ya kawaida, dawa ya pili, utaifunga kwenye mto unao
lalia, halafu dawa ya tatu utaiweka chini ya kitanda chako. Ndani ya siku mbili
hizi, kuna kitu utakiona ukiwa umelala usiku. Kitakujia katika ndoto. Kitu
hicho kina uhusiano na mwanaume unaye mtaka. Uki kiona kitu hicho tu, basi
haraka sana nipigie simu nikuelekeze kitu cha kufanya.. Nikazichukua hizo dawa
na kufanya kama nilivyo elekezwa.
NAMUONA “ K” KWENYE NDOTO.
Siku ya kwanza sikuona
chochote, ila usiku wa siku ya pili, nikiwa nimelala usiku, niliijiwa na ndoto
ya ajabu . Katika ndoto hiyo, nilimuona K akiwa anatembea kuja mahali kilipo
kibanda changu cha genge.Alipofika kwenye kibanda changu alisimama na
kuniulizia kama nina hiriki. Kabla sijamjibu, ndoto ikakatika ghafla… Nilipo
stuka na kutazama saa ilikuwa majira ya saa sita na ushee usiku.Hapo hapo
nikampigia simu Mungu wa Kabili na kumueleza nilicho kiona ndotoni…
Akaniambia vizuri sana, kisha
akaniuliza, je hilo eneo ambalo umemuona huyo mwanaume akiwa anatembea,
unalifahamu. Nikamjibu ndio nalifahamu. Akaniambia, kesho saa kumi na mbili
alfajiri, nenda kamwagie ile dawa niliyo kwambia uitunze chini ya kitanda.
Baada ya hapo akaninisisitizia, “ Ukiisha fanya nae mapenzi, uje unione haraka
iwezekanavyo, tufanye dawa za kumfunga..Nikafanya kama alivyo nielekeza,
alfajiri ya saa kumi na mbili, nikadamkia katika eneo hilo, kisha nikamwaga ile
dawa halafu baada ya hapo nikarudi zangu nyumbani kujiandaa na kufungua genge
langu.
NAINGIA KATIKA UHUSIANO WA
KIMAPENZI NA “K” MUME WA MTU.
Saa mbili asubuhi nilifungua
genge langu, nakumbuka siku hiyo ilikuwa Jumamosi. Mida ya kama saa nne hivi, K
alikuja hadi gengeni kwangu na kununua vitu mbalimbali vya genge, kama vile
karoti, nazi,pilipili manga nakadhalika na kurudi kwake.Baada ya kama masaa
mawili hivi, K alirejea tena pale gengeni kwangu, na kuchukua vitu vingine
zaidi, halafu akaomba namba yangu ya simu, aka save namba yangu na mimi
nikachukua yake, kisha akaondoka zake. Baada ya kama nusu saa hivi, K akaanza
kunitumia meseji za kunisifu.
Alianza kwa kuniambia mimi ni
mwanamke mchapakazi, najituma sana , nna hasira na maisha , nnafaa kuwa mama
kwa sababu hata mume akifa anakuwa na uhakika watoto wake anawaacha na mwanaume
imara.. Mwisho wa siku akanitongoza, na mimi sikulazia damu. Kesho yake, mimi
na K tukakutana kimwili kwenye hoteli moja iliyopo maeneo ya Mbezi Beach.Siku
hiyo K akaniambia niachane na kazi ninayo ifanya, atanitafutia biashara nzuri
ya kufanya, pia nihame pale nilipo kuwa nakaa, atanipangia nyumba inayo endana
na hadhi yake.
NAPEWA DAWA ZA KUMPUMBAZA MUME
WA MTU.
Mungu wa Kabili aliniambia,
nikisha fanya mapenzi na huyo mwanaume, niende kwake ili anipe dawa za
kumpumbaza. Nilipofika akaniambia, vitu vinavyo hitajika katika kutengeneza
hiyo dawa ya kumpumbaza huyo mwanaume, ni NYWELE ZA MWANAUME MWENDAWAZIMU,
NYWELE ZA MWANAUME ASIYE SIKIA ( KIZIWI ) , NYWELE ZA MWANAUME KIPOFU AU FIMBO
ILIYO TUMIWA NA MWANAUME KIPOFU, KAMBA ILIYO TUMIKA KUMFUNGA KONDOO , pamoja na
UCHAFU WA JALALANI.
Vitu vyote hivyo vilitafutwa
vikapatikana, vikachanganywa na dawa nyingine za kichawi,kisha vikatumika
kutengeneza uchawi. Nikaambiwa nitamuwekea kwenye maji ya kuoga na nyingine
nitamuwekea kwenye chakula .Halafu nikapewa na kibuyu, ndani ya kibuyu kile
kulikuwa na kipande cha nyama. Mganga akaniambia hiyo ni nyama ya ndege wa
usiku mwana wa jinni, ambayo baadae nilikuja kujua kuwa ni Bundi wa Kichawi,
ambae ni tofauti na bundi wa kawaida. Mganga akaniambia utapika nyama, katika
nyama utakayo pika ambayo utamuwekea ndumba, mwanaume wako, utachanganya na
nyama hiyo, pamoja na kucha zako, na nywele zako za siri.Nilipo rudi nyumbani,
nikafanya kama nilivyo elekezwa. Baada ya kufanya uchawi huu, K alikuwa kama
mwendawazimu kwangu, hakusikia wala kuambiwa na mtu yoyote Yule. Akawa anafanya
kila ninacho taka akifanye mimi. Akaanza kuwa ananipa mali zake, magari,
viwanja, nyumba, biashara pamoja na miradi yake..
NATEGA UCHAWI WA KUTOA MIMBA YA
MKE MWENZANGU.
Mapenzi yangu na K yalipamba
moto, nyumba aliyo nipangishia haikuwa mbali sana na mahali alipokuwa anaishi
yeye na mkewe, wao walikuwa wanaishi Tabata Mawenzi, mimi akanipangia nyumba
nzima Tabata Kimanga. K alihama kwa mke wake, akawa anaishi nyumbani kwangu.
Taarifa za K kuishi na “mchepuko” zilimfikia mke wake, lakini hakuwa na kitu
cha kufanya kwa sababu K alikuwa ndio anamuweka mjini yeye na familia yake na
mwanamke alikuwa mama wa nyumbani tu.
Mara nyingi K alikuwa
ananishauri amfukuze mke wake, ili nikaishi nae kwenye nyumba yake, ili
kuninonyesha kuwa ananipenda sana na mimi ndio kila kitu kwake. Ila kuna kitu
kimoja, alinifundisha Mungu wa Kabili, kwamba unapokuwa mchawi, unatakiwa uwe
mnafiki. Usiache kabisa watu wajue kwamba una jambo Fulani kwa sababu ya uchawi
.
Hivyo nikawa najifanya kama
namuonea huruma mke wa K lakini moyoni nilikuwa nataka afukuzwe mimi nikakae,
pale.Kuna kitu kimoja kilikuwa kinaniumiza moyo. Mke wa K alikuwa na ujauzito
wa kama miezi mitano hivi. Sikutaka mwanamke huyo azae na K kwa sababu nilijua,
angezaa na K mtoto angekuwa kiunganishi kwao, Mimi nilitaka K akisha achana na
mke wake, basi iwe ndio moja kwa moja na kusiwe na chochote cha kuwaunganisha.
Hivyo nikaanza kupanga njama za kuharibu ujauzito wa mke wa K kwa kutumia
uchawi.Suala hili nikalifikisha kwa Mungu Wa Kabili.
Mungu wa Kabili akaniambia
nitakupa dawa utaenda kutega kwenye mlango wake. Mti huo ni wa ajabu sana. Jina
lake linafanana na jina la moja kati ya wilaya zilizopo kusini mwa Tanzania
bara.Baada ya kupewa dawa hiyo, nikafanya ujanja nikaenda kuitega kwenye mlango
anaoutumia kupita. Alipo ruka mimba ikatoka. Kutoka kwa mimba ya mke wa K
kulinipa sababu ya kurudi kwa mganga kwa ajili ya kuwatenganisha kabisa K na
mke wake. Nilijua, majirani wangesema K kamuacha mke wake kwa sababu mke ana
matatizo ya uzazi.
NAMTENGANISHA K NA MKE WAKE.
Nikarudi kwa mganga ili tufanye
uchawi wa kumtenganisha K na mke wake. Mganga alichukua nyoya la ndege ambaye
simfahamu jina lake, pamoja na dawa ambazo sikuzijua pia, akachukua majina ya K
na mke wake, akaenda kuchoma jalalani. Alipomaliza hapo, tukaenda kaburini, kwa
ajili ya kuuzika rasmi uhusiano wa K na mke wake. Baada ya kuzika uhusiano wa K
na mkewe, yalifanyika matanga kwa ajili ya kuomboleza “kifo’ cha ndoa ya K.
Mganga alisema, kitu kilicho kufa, kinastahili kupewa maziko ya heshima. Usipofanya
hivyo, roho ya kitu hicho itakusumbueni.Niliporudi mjini nikakuta mke wa K
kaondoka kwake, kahamia kwa dada yake. Mimi nikahamia moja kwa moja kwa K
nyumba niliyokuwa nimepangiwa Kimanga nikamuweka mdogo wangu wa kiume
.NAANZA KUFUATILIWA NA NDUGU
WA MKE WA ‘K’.
Ndugu wa mke wa K
hawakufurahishwa na kuachana kwa K na mkewe, hivyo wakafanya kila juhudi
kuwapatanisha, lakini msimamo wa K ulikuwa ni ule ule, kwamba hataki tena kuwa
na mke wake na ameamua kuishi na mwanamke mwingine ambae ni mimi. K alikataa
hata kushiriki kwenye vikao vya usuluhishi. Ndugu wote wa upande wake na upande
wa mke wake wakawa wamemsusia K.Watu wawili hawakutaka kukubaliana na matokeo.
Nao ni baba wa mke wa K, pamoja na kaka mkubwa wa mke wa K.
Watu hawa waligundua kilichotokea
kati ya K na mke wake sio hali ya kawaida bali ni nguvu za ushirikina. Hivyo
wakaamua kutafuta suluhisho kwa waganga. Walipo zunguka kwa waganga,
hawakufanikiwa, hadi wakakata tamaa kunidhuru kwa njia ya uchawi.Mwisho wa siku
wakaamua, kunikodia majambazi, waje wanipige risasi. Walijua mimi ndio kikwazo
kwa mtoto wao kurudiana na mume wake, hivyo njia pekee ikawa ni kifo tu.
Nilisurika kuuwawa na majambazi
zaidi ya mara saba. Wakati huo Mungu wa Kabili alikuwa Lubumbashi nchini Kongo
kwa shughuli zake. Alipo rejea nikamfuata kwa ajili ya kuomba ulinzi wake.Kuna
mnyama mmoja wa mwituni, ana ndimi mbili, yani ulimi wake una ndimi mbili,
Mungu wa Kabili akatafuta ulimi wa mnyama huyo, mavi ya chatu pamoja na dawa
zingine anazo zijua, lengo lake likiwa ni kuwatenganisha na kuwafarakanisha
baba na kaka wa mke wa K ili wasipate nafasi ya kukaa pamoja na kunifuatilia.
Halafu baada ya hapo, akaagiza
nipeleke mchanga wa kwenye kaburi la mtu aliyepita duniani bila kuonekana, ili
anitengenezee dawa ya kuwafunga adui zangu wasinione. Pamoja na hivyo, akanipa
hirizi iliyo tengenezwa kwa Mti Mkuu wa Wachawi.Katika ulimwengu wa wachawi,
mtoto aliye kufa akiwa tumboni kwa mama ake. Huitwa mtu aliyepita duniani bila
kuonekana.Nilivyo mpelekea udongo wa kwenye kaburi la mtu aliye pita duniani
bila kuonekana, mganga akauchukua akafanya ulozi wake, halafu tukaenda wote
hadi mtoni, akaenda akatega ndumba zake, pale, kesho yake tukakuta chura
amenasa pale.Wachawi wana amini, roho za watoto wanao kufa kabla hawajazaliwa,
huwa zinaenda kuishi mtoni kama Chura. Lakini sio chura wote wapo hivyo, ni
baadhi. Waganga wana utaalamu wao wa kujua chura yupi anahusika hapo.Basi kaka
na baba wa mke wa K, walikosana kwa ugomvi mkubwa, kiasi mtoto akawa anamtukana
baba ake mzazi tusi la mama. Na kuhusu vitisho vya majambazi havikutokea tena
NATUMIA UCHAWI KUOKOA UHUSIANO
WA KAKA ANGU.
Kaka angu ambaye nimempita
miaka mitano, alikuwa anaishi kwenye nyumba ambayo K alinipangia. Nyumba hii
ilikuwa maeneo ya Tabata Kimanga. Kaka angu alikuwa katika uhusiano wa
kimapenzi na mwanamke ambaye alikuwa Baa Medi kwenye bar inaitwa Mawenzi
Garden. Alimuachisha kazi ya ubaa medi baada ya mimi kumuwezesha kiuchumi
kutokana na hela na mali nilizo hongwa na K pamoja na kumpa mradi mmoja wa K
ausimamie. Mdogo wangu alimpenda sana mwanamke huyo .Ila tatizo moja la
mwanamke huyo, alikuwa na tabia ya umalaya. Umalaya ulikuwa kwenye damu yake .
Basi siku moja mdogo wangu
alikuja kwangu kunishitakia kuhusu tabia ya wifi yangu. Mdogo wangu alikuwa
anampenda sana mwanamke huyo, na alikuwa hawezi kumuacha kwa sababu yoyote ile,
ila alikuwa anamuumiza sana kwa sababu ya tabia yake ya umalaya.“ Ninampa kila
kitu huyu mwanamke, ninampa hela, nimemfungulia biashara, nimempa gari,
nawasomesha wazazi wake na kusaidia familia yake,.
Lakini haridhiki tu, mwisho wa
siku anatumia hela ninazo mpa kuhonga wanaume wengine.. ( HELA , GARI NA VITU
VYOT AMBAVYO MDOGO WANGU ALIKUWA AKIMPA WIFI YANGU, VILIKUWA MALI YA K ALIZO
CHUMA KWA JASHO LAKE NA MKE WAKE)Nilimuonea huruma sana mdogo wangu, na
nikaamini sio akili yake ila atakuwa amerogwa na mwanamke Yule. ( UNAJUA UKIWA
MSHIRIKINA, KILA KITU UNAKUWA UNAAMINI KIMESABABISHWA NA USHIRIKINA )
Nikamwambia mdogo wangu
usijali, kesho nitakwenda Bagamoyo kwa mtaalamu wangu, nitamuelezea tatizo lako,
halafu nitamsikia atakacho niambia, nitakujulisha, ila usijali kama mwanamke
huyo amekufanyia mambo ya Kiswahili, itajulikana tu na utakuwa huru.Nilipo fika
kwa Mungu wa Kabili, nikamueleza kila kitu, akaniomba majina ya mdogo wangu
pamoja na jina la huyo wifi yangu, akatazama kwenye radar zake, halafu akacheka
sana.Mungu wa Kabili akaniambia, hakuna haja ya kumfunga mwanamke huyu. Huyu
mwanamke ana sumbuliwa na damu ya umalaya.
Umalaya upo kwenye damu yake.
Hata tukimfunga kwa mdogo wako, tutakuwa tunajisumbua tu, atampenda sana mdogo
wako, lakini atatoka nje tu kwa wanaume wengine. Hapa cha msingi, afanyiwe dawa
ya kumfanya aache umalaya.Mungu wa Kabili akachukua dawa moja inaitwa GEGEZI.
Hii Gegezi ina ukubwa kama tunda linaitwa DADANSI na ina mibamiba.Halafu
akachukua dawa nyingine ambayo ni chakula cha ndege mmoja wa porini. Ndege huyo
simkumbuki jina lake, ila ni mweusi, ana mdomo mrefu, ndege huyu akilia,
vinyonga wote waliopo katika eneo hilo wanakimbia, huwa anakula vinyonga pia.,
Sasa ndege huyu huwa anakula
majani ya mti Fulani wa porini ambao nimeusahau jina lake, hayo majani ndio
ambayo Mungu wa Kabili aliya chukua. Kitu kingine akachukua majani Fulani hivi,
hayo majani ndio majani pekee yanayo liwa na mnyama wa porini ambae chakula
chake kikuu ni nyama.Pamoja na dawa hizo akachanganya na dawa zake nyingine
ambazo sikuweza kujua ni dawa gani, halafu akaagizwa itafutwe minyoo ipatayo
saba. Vito vyote hivyo vikaunguzwa pamoja kwenye chungu, hadi vikawa unga unga
halafu vikachanganywa na mafuta ambayo sikujua ni mafuta ya kitu gani.
Mungu wa Kabili akanipa dawa
hiyo akaniambia mpelekee kaka ako. Mwambie akiwa anafanya mapenzi na huyo
mwanamke wake, afanye ujanja wake, achovye kidole chake kwenye hiyo dawa halafu
akichomeke kwenye uke wa mwanamke huyo.Tangu siku hiyo, mwanamke huyo hatokuwa
Malaya tena . Nikafanya kama alivyo nielekeza na tangu mdogo wangu afanye
hivyo, sikuwahi kumsikia tena akinipa kesi za wifi yangu, zaidi ya kumsifia
mpenzi wake ametulia. Mwisho wa siku walifunga ndoa na kuzaa watoto.
NAMTEKA KICHAWI KIJANA WA
KIARABU.
Nilimroga K kwa sababu ya pesa
zake. Nikiwa kama mwanamke kamili, nilihitaji kuwa na mwanaume ninaye mpenda
kutoka moyoni mwangu. Nataka nitoe funzo moja kwa wanaume, mnajua kila mwanamke
alie olewa ambae hajaokoka huwa ana wanaume wawili. Mwanaume wa kwanza ni
mwanaume ambae yupo nae katika ndoa, na mwanaume wa pili ni mwanaume ambae
alitamani awe nae katika ndoa. Hivyo ndivyo ilivyo kuwa kwangu.Sasa basi, kuna
kijana mmoja wa kiarabu ambae nilikuwa namzidi umri kwa miaka minane. Kijana
huyu aliishi mtaa wa pili kutoka nyumba niliyo kuwa nikiishi na K.
Nilitokea kumpenda sana kijana
huyo lakini sikuwa na namna ya kumuanza, mnajua mwanamke kumtongoza mwanaume
sio kazi rahisi. Nikaona isiwe tabu nikaamua kwenda kwa Mungu wa Kabili, ili
anipe ndumba za kumnasa kijana huyo ambae kwa jina aliitwa Feisal.Nilipo fika
kwa Mungu wa Kabili akaniambia “ Inaonekana wewe ni mtundu mtundu sana,. Halafu
naona una mambo mengi. Sasa nitakutengenezea uchawi, ambao utakuwa unautumia
mwenyewe kumnasa mwanaume yoyote unae mtaka. “. Mungu wa Kabili akaniambia,
njia hiyo itakuwa bora kuliko mimi kuwa naenda kumuona kila mara kwa jambo lile
lile.Mungu wa Kabili akaniambia, nitafute kopo linalo tumika chooni, nitafute
nguo za marehemu.
Hapa simaanishi nguo za maiti,
la hasha nina maanisha nguo za marehemu.Mfano wake ni kwenu kuna mtu amefariki,
nguo zake zimegawiwa kwa ndugu, jamaa na marafiki, sasa nguo hizo ndio anazo
zitaka.Mungu wa Kabili, akaniambia niwe na uhakika kwamba nguo nilizo pewa ni
nguo za marehemu kweli, hilo la kwanza, lakini pili niwe na uhakika kwamba
marehemu huyo alikufa kifo cha Mungu na sio kachukuliwa msukule.Nikamuuliza
nitajuaje kuhusu mambo hayo, akaniambia ni rahisi sana. Wewe ukizipata nguo za
marehemu, au mtu atakae kuuzia nguo za marehemu, basi akuonyeshe mahali lilipo
kaburi la marehemu, halafu utakuja kwangu nikuelekeze cha kufanya.( KATIKA
ULIMWENGU WA WACHAWI, NGUO ZA MAREHEMU NI BIASHARA KUBWA SANA, KUNA WATU
WANAISHI KWA KUFANYA BIASHARA YA KUUZA NGUO ZA MAREHEMU MBALIMBALI..MIMI
MWENYEWE NILIUZIWA NGUO ZA MAREHEMU KWA BEI MBAYA ).
Baada ya kufanikiwa kupata nguo
za marehemu, pamoja na kuonyeshwa mahali lilipo kaburi la huyo marehemu,
nilirejea kwa Mungu wa Kabili.Mungu wa Kabili alizichukua zile nguo, akakata
kipande kidogo kwenye shati moja, akapaka mafuta ambayo sikujua ni mafuta ya
nini, akazifunga kwenye kitambaa chekundu, akaweza kwenye kibuyu, ndani ya
kibuyu hicho akaweka yai la kuku mweusi, sindano saba pamoja na mafuta mengine
ambayo sikujua ni mafuta ya nini ila wao wachawi na waganga wanayaita mafuta ya
usiku, kisha akakifunga kile kibuyu, halafu akanikabidhi, akaniambia, ikifika
usiku wa saa moja , nenda hadi kwenye hilo kaburi, kisha ukiweke kibuyu hicho
juu ya hilo kaburi kwa kukilaza., halafu asubuhi pita katika kaburi hilo
uangalie kwa makini kibuyu hicho, ukikikuta bado kimelala kama ulivyo kiacha
basi ujue huyo marehemu kweli amekufa kifo cha Mungu, lakini ukikuta
kimesimama, basi marehemu huyo bado yupo hapa hapa duniani, amechukuliwa
msukule.Nikafanya kama alivyo niagiza, na kweli kesho yake nikakuta kibuyu
kimelala kama nilivyo kiweka.
Mungu wa Kabili akaniambia nguo
hizo zinafaa kwa ajili ya kutengeneza dawa hiyo.Basi akachukua hizo nguo,
akaziunguza kwenye chungu cheusi pamoja na dawa nyingine kama aina kumi na
mbili, halafu akazihifadhi kwenye kibuyu na kunikabidhi, pamoja dawa zingine
kwenye vifuko vitatu.Akaniambia, ukimtaka mwanaume yoyote Yule, utamuita kwa
kutumia dawa hii… Mwanaume utakae muita sauti yako ataisikia na kuitii mara
moja kama ambavyo marehemu huyo alivyoitwa na Mungu na kuitii sauti yake.
Mungu wa Kabili akaniambia huo
ni uchawi mkubwa sana katika mapenzi, hakuna mwanaume nitakae muita na akakataa
kuitika. Uchawi huu hautumiki katika mapenzi tu, hata kama mambo mengine,
ilimradi unacho taka wewe ni kumuita mtu.Kitu kingine akaniambia, ukimuita
mwanaume kwa kutumia uchawi huu zaidi ya mara saba, halafu akakataa kuitika,
basi jua kwamba mwanaume huyo kinga yake ni kubwa sana.Sasa basi ukisha
ligundua hilo, unatakiwa kutuma nyoka wa kichawi kuua kinga ya mwanaume huyo.
Ukisha ua hiyo kinga, muite
tena mwanaume huyo na atakuja haraka sana.Nyoka huyu sio nyoka wa kawaida kama
nyoka wengine. Ni nyoka wa kichawi. Ni jinni. Mungu wa Kabili akanikalisha
kwenye kigoda na kuniambia, “ Nitamtengeneza nyoka huyu, halafu nitakukabidhi,
umtunze vizuri kwa kufuata masharti yake…”Katika kumtengeneza nyoka wa kichawi,
Mungu wa Kabili akachukua kitovu cha mtoto.
(
KUWENI MAKINI SANA NA MAHALI MNAPOVITUPA VITOVU VYA WATOTO WENU.. KATIKA
ULIMWENGU WA WACHAWI VITUVO VYA WATOTO NI BIASHARA KUBWA SANA… KITOVU CHA MTOTO
KINAPOENDA KUTUPWA, AMA KUFUKIWA, KATIKA WATU WANAO PEWA JUKUMU LA KUVITUPA,
HUWA KUNA MMOJA WAPO ANAWEZA KUWA SIO MUAMINIFU, HUENDA KUFUKUA MAHALI
KILIPOFUKIWA NA KWENDA KUKIUZA KWA WACHAWI NA WAGANGA )
Alipochukua hicho kitovu,
akakifunga kwenye mti wa mnyonyo, halafu akanyunyizia dawa kutoka kwenye
vichupa kama saba. Baada ya hapo akachukua uzi mwekundu, akafunga vifundo saba
kwenye kamba hiyo, halafu akatupa kwenda chini, ilipotua tu, ikageuka kuwa
nyoka.
Akamshika huyo nyoka,
akamuhifadhi kwenye kibuyu cheusi, chenye shanga juu, akafunga na kitambaa
cheusi na kunikabidhi.. Akanielekeza jinsi ya kumtuma nyoka huyo kufanya kazi
mbalimbali pamoja na masharti yake.Kuhusu lile kopo la chooni, Mungu wa Kabili
akaniambia amelitumia kutengeneza dawa ya kujua siri za watu. Dawa hiyo
itanisaidia kujua kama mwanaume niliye nae ana hela au hana hela, ana mke au
hana mke. Ana watoto au hana watoto.Kingine akanikabidhi ua ambalo natakiwa
kulipanda nyumbani. Kupitia ua hilo nitakuwa ninajua kama mwanaume ambae nipo
nae amepata hela au la.Kitu cha mwisho, akaniambia, kwa sababu nnaonekana
nnapenda sana wanaume, inabidi anipe dawa ya kuwatengeneza wanaume nitakao kuwa
nao na kuwafanya kutokuwa na uwezo wa kufanya mapenzi na wanawake wengine
isipokuwa mimi tu. Hii itasaidia kuniepusha na magonjwa kama vile ukimwi
nakadhalika.
Mungu wa Kabili akanipa mti
mmoja mrefu, akaniambia katika mti huo, utatumia zaafarani nyekundu au ya
njano, kuandika majina ya wanaume wote ambao upo nao kimapenzi pamoja na jina
lako, ukisfanya hivyo, nenda kautegeshee barabarani, ukishagongwa na gari tu,
basi wanaume hao watakuwa wakikutana na wanawake wengine, uume wao unakuwa
haufanyi kazi.
Nilivyo rudi nyumbani nikafanya
kama nilivyo elekezwa na kweli Yule kijana alikuja mara moja tangu nilipo
muita. Nilifurahi sana kumpata Feisal. Pamoja na kwamba nilikuwa nimemuita
kichawi ila nilikuwa namuheshimu sana kwa sababu nilikuwa nampenda toka moyoni
mwangu.
Baada ya kama wiki mbili tangu
nianzee uhusiano wangu na Feisal, nikagundua Feisal ana tatizo la ukosefu wa
nguvu za kiume. Uwezo wake kitandani ulikuwa mdogo sana.Kama kawaida yangu
nikaenda kumuona Mungu wa Kabili. Mungu wa Kabili akanipa dawa moja inaitwa
KISHINDO. Akaniambia utakuwa unachemsha unampa anakunywa glasi moja asubuhi na
nyingine anakunywa jioni, kwa siku kumi mfululizo.
Nikafanya kama alivyo
nielekeza. Baada ya kumpa Feisal dawa hiyo, nilijilaumu kwanini nilifanya
hivyo. Uwezo wake kitandani ulikuwa wa ajabu, alikuwa anashiriki tendo kwa muda
mrefu sana na alikuwa akirudia mara nyingi bila kuchoka…
NAMFANYIA VITUKO K
Katika muda wote huo, nilikuwa
bado ninaishi na K kwenye nyumba yake ya Tabata Mawenzi. K alikuwa kama
Ndondocha kwangu. Kwanza nilikuwa simpi unyumba na nilikuwa nafanya kila kitu
ninacho taka kukifanya tena mbele yake.Feisal alikuwa anakuja nalala nae
chumbani, K analala pepe yake kwenye chumba kingine. Alikuwa anafanya kazi zote
kama vile kufua, kufanya usafi na kila aina ya kazi ambayo houseboy anatakiwa
kuifanya.
Na katika kipindi hiki K
alikuwa ameshafukuzwa kazi kutokana na uzembe kazini. Mimi mwenyewe nilimpiga
marufuku kwenda kazini kwa mwezi mmoja, nilimwambia achague kitu kimoja kati ya
kwenda kazini au kufanya kazi zangu.Sasa basi nikawa namfanyia K vituko, lengo
langu nikitaka aondoke mwenyewe aniachie nyumba na mali zake. Hakuwa na faida
yoyote tena kwangu. Kazi ameshafukuzwa , mali zake zote pamoja na biashara zake
ninazimiliki mimi.Basi kila nilipokuwa nikifanya mapenzi na Feisal nikawa
napiga kelele ili kumuudhi K.
Na hivi Feisal alikuwa anatumia
muda mrefu basi na kelele zangu zikawa za muda mrefu. Lakini wapi, K wala hata
hakuonyesha dalili ya kwamba anaweza kuondoka , undondocha ulikuwa umetamalaki
kwenye kichwa chake.Kwa kutumia ndumba hizo nilizo pewa na Mungu Wa Kabili,
niliwateka kichawi wanaume wengi na kuvunja ndoa nyingi sana.
K ANAAMUA KURUDI KIJIJINI
Nilipoona K hana dalili ya
kuondoka pamoja na kumfanyia vituko lukuki, nikaona niende kwa Mungu wa Kabili
ili kama kuna uwezekano wa kumfukuza K kichawi.Nilipofika kwa Mungu wa Kabili,
akafanya dawa zake, halafu ikatengenezwa ngalawa ndogo, nikaambiwa nipeleke
nguo yoyote ya K . Nguo ya K ikafanyiwa uchawi halafu ikafungwa kwenye hiyo
ngalawa, tukaenda baharini kutegea wakati bahari imesafiri tukaenda kuiweka
ngalawa , maji yalipokuja yakaondoka na hiyo ngalawa, kesho yake tu, K mwenyewe
akasema anataka kwenda kusalimia kijijini kwao amepakumbuka. Nilifurahi sana
niliposikia hivyo, nikamfungia nguo zake, nikampa na nauli pamoja na hela ya
kula njiani.
Kalivyo rudi kwao, baadhi ya
ndugu zake hawakuridhishwa na hali ya K pamoja na maelezo yake. Mtu aliyekuwa
tegemeo la ukoo mzima, ghafla anarudi kijijini akiwa hana kitu na maelezo yake
yanatatanisha. Wakaamua kufunga safari hadi mjini ili kufuatilia mali za ndugu
yao. Nilipo pata taarifa zao, nikaenda kuwashitaki kwa Mungu wa kabili, wote
walipeperuka na sikusikia chochote kuhusu watu hao.
NAINGILIA NDOA YA WALOKOLE.
Nilitokea kumtamani mwanaume
mmoja mlokole alieishi mtaa wa pili kutokea nilipokuwa naishi. Huyu nilimpenda
kama nilivyo mpenda Feisal. Alikuwa mkaka mzuri anae jipenda sana. Kwa jina
aliitwa Erasto. Kikwazo kikubwa kwa Erasto ilikuwa, kwanza alikuwa ameokoka na
pili alikuwa na mke ambaye alikuwa ameokoka pia. Mke wa Erasto alikuwa na
ujauzito mkubwa tu wa kama miezi mitano au sita .
Nasema kuokoka ilikuwa kikwazo
kwa sababu Mungu wa Kabili Alisha nishauri niwe makini sana na walokole kwa
sababu wana nguvu za ajabu. Ila akaniambia kuna walokole wa waina mbili., mlokole
wa ukweli na mlokole feki. Hivyo basi
kama umemempenda mwanaume wa kilokole, unatakiwa kwanza umpime kichawi kujua
kama ni mlokole wa ukweli ama mlokole feki.
Akaniambia uchawi unao tumika
kupima nguvu ya mlokole, sio uchawi wa kitoto, hauwezi kufanywa na mtu yoyote,
akaniambia kama itatokea nimempenda mwanaume wa kilokole, basi niende kwake
halafu yeye atampima kama mlokole huyo ni orijino au feki..
Kama ni orijino una achana nae
kwanza unatafuta njia nyingine ya kumpata, lakini kama ni feki,unamvuta kama
watu wengine.Akaniambia, ukimpenda mwanaume wa kilokole orijino ni bora utumie
njia za kawaida kumteka, kuliko njia za kichawi, kwa sababu kwa njia za
kawaida, ataishia kukukemea tu,. Lakini kwa njia ya uchawi, utapigwa shot.
Hakuniambia ni shoti gani.
TUNATUMIA UCHAWI KUPIMA ULOKOLE
WA ERASTO.
Ili kujua kama mlokole ni
orijino au feki, wachawi hutumia nzi. Hivyo basi Mungu wa Kabili alianza
kufanya uchawi ili kupima kama Erasto ana nguvu za Mungu au hana nguvu za
Mungu.Siku hiyo Mungu wa Kabili akachukua bakora ya kichawi ambayo
imetengenezwa kwa mti wa Mkomoro, Mganga akaniambia mti huo wa mkomoro ni mti
wenye nguvu nyingi sana za kichawi na wachawi huutumia kwa mambo mengi ikiwa ni
pamoja na kufufua wafu.Mungu wa Kabili akaanza kwa kuwaita inzi na kisha
kuwatuma waende kwa Erasto ili kujua kama ana nguvu za Mungu au la. Lilikuja
kundi la nzi wengi, na walipo tua tu kwenye fimbo yake wote wakapasuka pale
pale.
Mungu wa Kabili akaniambia kwa
kunisisitiza, achana kwanza na huyu Erasto, kesho ninasafiri kwenda Mkuranga ,
nitakuwa huko kwa siku saba tunaenda kupika uganga . Nitakapo rudi tutaangalia
njia nyingine ya kumteka Erasto.Waganga na wachawi huwa wanakuwaga na MWAKA WA
UCHAWI ama MWAKA WA UGANGA, kama ambavyo kuna MWAKA WA FEDHA, MWAKA WA MASOMO
nakadhalika.
Unapofika mwaka wa uganga,
waganga hukutana mzimuni na kupika uchawi, ambao huuzwa kwa waganga mbalimbali.
Jambo hilo hufanyika kila mwaka.Mungu wa Kabili alikuwa anaelekea Mkuranga kwa
ajili ya kusimamia zoezi la upikaji wa uchawi unaoitwa MANGUBE. Kwa hiyo Mungu
wa Kabili akaniambia nisubiri kwanza mpaka wiki mbili zipite ndio tuje tukae
tupange cha kufanya juu ya Erasto, kwa sababu baada ya kutoka Mkuranga alikuwa
anaelekea Liwale Lindi. Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na maagizo ya
Mungu wa Kabili.
NAMTUMIA ERASTO NYOKA WA
KICHAWI.
Baada ya siku tatu uvumilivu
ukanishinda, nikaamua liwalo na liwe, kama kuna baya litanitokea, Mungu wa
Kabili atanisaidia. Usiku wa saa sita siku hiyo, nikamchomea Erasto, dawa ya
kumvuta kwangu kichawi. Kwa kawaida nikishachoma dawa, usiku huwa naota nafanya
mapenzi na mwanaume nilie mchomea dawa na kesho yake, kabla ya saa sita
mwanaume huyo huwa ananitafuta, lakini kwa Erasto ikawa tofauti.
Sikuona chochote. Nikachoma kwa
siku saba mfululizo hakuna chochote. Nikakumbuka Mungu wa Kabili aliniambiaga
kwamba, kama nikichoma dawa ya kumuita mtu na mtu huyo asije, basi nijue kuwa
mtu huyo ana kinga kubwa, kwa hiyo natakiwa nimtumie nyoka wa kichawi, nyoka
huyo ataenda kuvunja kinga ya mtu huyo.Siku hiyo usiku wa saa sita, nikaenda
kuchukua kile kibuyu ambacho kilitumika kumuhifadhi Yule nyoka, nikamtuma nyoka
huyo aende kuigonga na kuivunja kinga ya Erasto. Nilipomaliza kunena maneno
yangu nikafungua kile kibuyu ili nyoka atoke, nyoka alipotoka akanigonga kwenye
mguu na kutokomea.Nilipiga kelele za ajabu, house girl wangu akaenda kuwaamsha
majirani na kupiga simu ya kaka angu, nikapelekwa hospitali, hospitali
nikapimwa lakini hakikuonekana kitu, wala haikuonekana kama nina sumu yoyote
mwilini, lakini nilikuwa nasikia maumivu makali sana yaliyokuwa yanakuja na kuondoka,
nikapewa dawa za kuzuia maumivu lakini wapi.
Ilipofika asubuhi maumivu
yakawa yameisha lakini nikawa nimepooza upande mmoja.Nikamwambia kaka angu
apige simu ya Mungu wa Kabili, lakini Mungu wa Kabili alipopigiwa na kuelezewa
kilicho tokea, akawa mkali sana, kwanza akasema alinionya nisifanye chochote
halafu pili akasema hawezi kunisaidia kwa namna yoyote ile.Sikuwa na jinsi
zaidi ya kumueleza kaka angu ukweli. Kilicho fuatia tukaanza kuzunguka kwa
waganga wa kienyeji kwa ajili ya tiba yangu lakini wapi. Baada ya wiki mbili
nilipelekwa kwa Mungu wa Kabili Bagamoyo angalu aione hali yangu ilivyo labda
anaweza kunionea huruma lakini, akakataa kata kata….
Msimamo wake ulikuwa ni ule
ule, nimefanya jambo ambalo alinikataza kulifanya na pia hana uwezo wa
kunisaidia. Zaidi aliniambia hatima yangu ni kifo.Tulizunguka kwa waganga wa
kila aina na kila sehemu lakini wapi hali yangu ikazidi kuwa mbaya.Siku moja
ndugu yangu mmoja wa upande wa mama angu, alikuja kuniona baada ya kusikia
nimepooza. Baada ya kumsimulia kuhusu kisa changu alisikitika sana.
Nikapelekwa kwenye kanisa moja
la kiroho na kuombewa. Siku tatu tangu nianze kuombewa nilitapika vitu vingi
sana vya ajabu ajabu, kama vile kucha, nywele, damu nakadhalika, na taratibu
hali yangu ikaanza kutengemaa na hatimaye nikapona kabisa.Namshukuru Mungu sasa
hivi nimeokoka, nimempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Mali za
K nimezirudisha na sasa ninaishi maisha yangu halali kwenye chumba cha kupanga
maeneo ya Mbezi Ya Kimara.Ninaumia sana moyoni kuona, nimeseababisha mateso kwa
wanawake wenzangu, nimevunja ndoa za watu. Nimeamua kumtumikia Mungu katika
maisha yangu yote.
Ninawaomba msamaha wale wote
nilio waharibia maisha.CHA MWISHO NA KIKUBWA.. NAWATAHADHARISHA WANAWAKE
WENZANGU KUHUSU WAGANGA WA KIENYEJI, HUSUSANI HUYU ANAEITWA MUNGU WA KABILI. NI
MTU HATARI SANA NA MCHAWI MKUBWA. NAOMBA MSIENDE KUFUATA MSAADA WAKE JAMANI KWA
SABABU NI MCHAWI.. NAMBA ZAKE ZA SIMU NI 0744 000 473. MSIPIGE NAMBA HIYO JAMANI, YATAWAKUTA KAMA YALIYO
NIKUTA MIMI. NIMEONA NIWEKE NAMBA ZAKE HADHARANI ILI MZIJUE NA KUJIEPUSHA NAZO,
KWA SABABU NAONA ANATANGAZWA NA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI. NAOMBA KILA
ATAKAE PATA UJUMB HUU, AMJULISHE NA MWENZAKEYESU AWAONGOZE NA AWALINDE.
Source
Mpekuzi 20th November
2017
Maoni