TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/J/112 28 Machi, 2018
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara
Zinazojitegemea, Taasisi za Umma mbalimbali Serikalini, Sekretarieti za Mikoa,
Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini – RITA,
anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza
nafasi wazi za kazi 113 kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.
1.1 AFISA UTAFITI KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURAL RESEARCH OFFICER
II) – NAFASI 4
(Agronomy Nafasi 1, Horticulture Nafasi 1, Agricultural Economics and
Agribusiness Nafasi 1 na Agriculture General Nafasi 1)
1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusaidia kuandika na kukusanya ripoti za utafiti wa Kilimo/Uchumi kilimo chini ya
maelekezo ya afisa utafiti mwandamizi,
ii. Kukusanya, kurekodi na kuchanganua takwimu za kazi za utafiti zinazoendelea,
iii. Kuhudhuria mikutano ya Kanda ya kuhuisha programu za utafiti,
iv. Kusaidia katika kuendesha semina na kuwaelekeza wakulima jinsi ya kutumia
teknolojia mpya kwa kuzingatia hali ya uchumi na mazingira yao,
v. Kutoa ripoti ya maendeleo ya utafiti na mapendekezo ya utafiti katika mikutano
ya kanda ya kuhuisha program za utafiti,
vi. Kufanya shughuli za utafiti chini ya maelekezo na uangalizi wa Afisa Utafiti
mwandamizi,
vii. Kuandika mapendekezo ya utafiti chini ya uongozi wa Afisa Utafiti Mwandamizi,
viii. Kuandika ripoti za miradi ya utafiti kwa ajili ya kupitishwa na Afisa utafiti
mwandamizi,
ix. Kufanya majaribio ya husishi ya kilimo ma mifugo katika mashamba ya wakulima
kwa kushirikiana na Maafisa Ugani na wakulima wenyewe na
x. Kufanya kazi zozote kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya Agronomy, Horticulture,
Agricultural Economics and Agribusiness na Agriculture General kutoka Chuo Kikuu
kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D.
1.2 DEREVA MITAMBO (PLANT OPERATOR) – NAFASI 1
1.2.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuendesha mitambo chini ya usimamizi wa Dereva mitambo mwenye uzoefu.
1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha nne ambao wana leseni Daraja la “G” ya
kuendesha Mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo hiyo, wenye
uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha
ajali.
1.2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS A.
1.3 FUNDI SANIFU - MAJENGO (TECHNICIAN II ARCHITECTS) – NAFASI 1
1.3.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya kazi kwa vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha kupata sifa za
kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili inayowahusu Wasanifu majengo,
ii. Kufuatilia upatikanaji wa taarifa na taaluma za usanifu wa majengo,
iii. Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposals) mbalimbali ya majengo
yanayowasilishwa Wizarani.
1.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:
i. Waliohitimu kidato cha iv na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka vyuo
vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani ya usanifu
majengo
ii. Waliohitimu kidato cha vi na kufuzu mafunzo ya ufundi wa miaka miwili kutoka
chuo kinachotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za usanifu majengo
iii. Wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Hatua ya I kutoka chuo cha ufundi
kinachotambuliwa na Serikali,
iv. Wenye Stashahada ya kawaida katika fani za ufundi kutoka Chuo kinachotambuliwa na
Serikali.
1.3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C.
1.4 MPISHI DARAJA LA II (COOK GRADE II) – NAFASI 1
1.4.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusafisha jiko
ii. Kupika chakula cha kawaida
1.4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua mwaka
mmoja katika fani ya ‘Food Production’ yanayotolewa na Vyuo vya Forodhani (Dar es
Salaam), Masoka (Moshi), Arusha Hotel, Y.M.C.A (Moshi), VETA (Mikumi) na Vision
Hotel (Dar es Salaam) au vyeti vingine vitakavyotambuliwa na Serikali na wenye
uzoefu wa kazi kwa muda usiopunguja miaka (3) mitatu.
1.4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali.
1.5 MJIOLOJIA DARAJA LA II (GEOLOGIST GRADE II) – NAFASI 1
1.5.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupokea na kufuatilia upatikanaji wa taarifa za utafiti wa mistari ya Uchungi na
Mitetemo katika utafutaji wa madini au petrol,
ii. Kukusanya na kuchambua taarifa za Mitetemo, mienendo na mabadiliko ya
miamba ardhini,
iii. Kutunza kumbukumbu za miamba, madini au petrol,
iv. Kutayarisha Rasimu za Taarifa za kitaalam na kuziwasilisha kunakohusika,
v. Kusimamia matumizi ya Vifaa vya Kitaalam na Utunzaji wake, na
vi. Anaweza kuongoza timu ya mafundi sanifu wanapokuwa katika shughuli za
utafutaji wa madini au petrol.
1.5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi katika Fani ya Jiolojia (pamoja na fani za
Jiofizikia au Jiokemia) au sifa nyingine zinazolingana na hizo kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.
1.5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E
1.6 MKUFUNZI DARAJA LA II - KILIMO (AGRICULTURAL TUTOR II) – NAFASI 1
1.6.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufundisha somo la kilimo katika vyuo vya maendeleo ya wananchi.
ii. Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
iii. Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
iv. Kutunza vifaa vya kufundishia
v. Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
vi. Kutoa Ushauri wa kitaalam
vii. Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
viii. Kutunga na kusahihisha Mitihani
ix. Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
katika jamii inayoizunguka chuo
x. Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya
chuo
1.6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/stashahada
ya juu katika somo la kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
1.6.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
1.7 AFISA MAMBO YA NJE DARAJA LA II (FOREIGN SERVICE OFFICER II) –
NAFASI 2
1.7.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa zinazohusu masuala ya kimahusiano ya
kimataifa.
ii. Kuhudhuria mikutano mbalimbali.
iii. Kuandaa mahojiano.
iv. Kufuatilia masuala mbalimbali ya kimataifa.
v. Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uchumi, siasa na jamii.
vi. Kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbali.
1.7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa (B.A) ambao wamejiimarisha (major) katika fani ya
uhusiano wa Kimataifa (international Relations), Sheria au Uchumi kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali. Aidha wawe
wamefanya na kufaulu mtihani unaotolewa Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.
1.7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
1.8 MTUNZA NYUMBA DARAJA LA III – NAFASI 1
1.8.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa vitanda,
ii. Kuhakikisha Usafi wa nguo (linen), Mapazia na mazulia,
iii. Kusimamia utunzaji wa bustani na ukataji majani (state lodge).
1.8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiliwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya Home
Economics au Sifa inayolingana na hiyo kutoka kwenye Vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali.
1.8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C.
1.9 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 1
1.9.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya uchambuzi wa nguo kwa ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na
kuzifungasha.
1.9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au mitatu
katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali.
1.9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS. C
1.10 MPIGA CHAPA DARAJA LA II (PRINTER GRADE II) – NAFASI 1
1.10.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kupanga ratiba ya kazi,
ii. Kuandaa Vifaa vya kufanyia Kazi,
iii. Kugawa kazi kwa Watumishi walio chini yake,
iv. Kufuatilia utekelezaji wa kazi zinazoendelea na kutoa taarifa kwa msimamizi wa
kazi,
v. Kutayarisha vielelezo (job jacket lay-out) kuhusu mtiririko wa kazi (Plan of production).
1.10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya kawaida ya Kupiga Chapa, kutoka Vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali wenye uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3).
1.10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C
1.11 MPIGA CHAPA MSAIDIZI (ASSISTANT PRINTER) – NAFASI 1
1.11.1 MAJUKUMU YA KAZI
Mtumishi katika daraja hili atakuwa katika mafunzo ya kazi chini ya usimamizi wa
Wapiga Chapa wenye uzoefu na kupangiwa Kazi zifuatazo;
i. Kukunja karatasi ngumu na kutengeneza ‘covers’ za vitabu, majarida, madaftari
katika mahitaji mbali mbali kwa kugandisha, kuweka pamoja au kushona katika
hali mbalimbali za ubora,
ii. Kukarabati vitabu, kumbukumbu mbalimbali au majarida kwa kuyawekea gamba
jipya au kurudisha katika hali yake ya mwanzo kutegemea na kifaa hicho
kilivyoharibika,
iii. Kupanga vifaa vilivyotengenezwa katika makasha kwa vipimo vyake au katika
seti,
iv. Kuendesha mashine za kukata karatasi/ kupiga Chapa/ Mashine za Composing,
kushona au kugandisha vitabu, majarida, madaftari na vifaa vingine vinavyokuwa
vimetakiwa kwa mtindo wa ubora wake,
v. Kupanga karatasi zitakazochapwa kwa hesabu ya kila kitabu, jarida, daftari na
vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa pamoja.
1.11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au cha Sita waliofaulu masomo ya Sayansi au
Sanaa, wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la I (Trade Test Grade I) katika
Lithography/ Composing/ Binding/ Machine Minding, au waliohitimu mafunzo ya miaka
miwili ya Kupiga Chapa.
1.11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B
1.12 MHUDUMU WA JIKONI DARAJA LA II (KITCHEN/ MESS ATTENDANT) –
NAFASI 5
1.12.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusafisha Vyombo vya kupikia.
ii. Kusafisha Vyombo vya kulia chakula.
iii. Kusafisha Meza itumiwayo kwa kulia chakula.
iv. Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya Mpishi na Mezani.
v. Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia.
vi. Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.
1.12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua
miaka mitatu.
1.12.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A
1.13 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 51
1.13.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
vi. Kufanya usafi wa gari na,
vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
1.13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha (IV) na leseni ya Daraja E au C1 ya
uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila
kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic
Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Waombaji wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.
1.13.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B.
1.14 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 15
1.14.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu;
ii. Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha;
iii. Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu;
iv. Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki; na
v. Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
1.14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na Bodi
ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
1.14.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B
1.15 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III (BASIC TECHNICIAN) – NAFASI
22
1.15.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
ii. Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
iii. Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
iv. Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
v. Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
vi. Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
vii. Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
viii. Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
ix. Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
x. Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya
Nchi
xi. Kudhibiti wanyamapori waharibifu
xii. Kudhibiti moto kwenye hifadhi
xiii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
1.15.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya Uhifadhi
Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha
Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.15.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali
1.16 MHANDISI RADIO DARAJA LA II (RADIO ENGINEER II) – NAFASI 1
1.16.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Uendeshaji wa mitambo ya Radio chini ya usimamizi wa wahandisi wazoefu.
ii. Matengenezo madogo madogo ya mitambo ya Radio.
iii. Anaweza kuteuliwa kuwa kiongozi wa zamu “Shift Leader”.
iv. Kuchunguza, kuchambua na kurekebisha mitambo ya Radio
v. Kusimamia na kuongoza Mafundi Mitambo walio chini yake.
1.16.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali katika fani ya Uhandisi wa Radio.
1.16.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS. E.
1.17 TABIBU DARAJA LA II (CLINICAL OFFICER II) – NAFASI 1
1.17.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kazi zote zinazofanywa na Tabibu Msaidizi,
ii. Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida,
iii. Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo,
iv. Kutoa Elimu ya Afya kwa jamii,
v. Kushiriki katika kupanga na kutekeleza Huduma za Afya ya msingi,
vi. Kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za afya na mfuko wa
afya ya jamii,
vii. Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma,
viii. Kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji,
ix. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
1.17.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne (IV) au sita (VI) waliofaulu Kozi ya Stashahada
ya Utabibu ya miaka miwili (kidato cha sita) au miaka mitatu (kidato cha nne) katika
Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.17.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya vya Serikali .
.
2.0 WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI – RITA
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini – RITA ni Wakala wa Serikali ulianzishwa chini ya
Sheria ya Bunge Na.30 ya Mwaka 1997 kufuatia Tangazo la Serikali Na. 397 ya tarehe
2/12/2005. RITA Ina jukumu la kuhakikisha ufanisi katika usimamizi wa taarifa ya
Matukio Muhimu ya Binadamu na huduma za Ufilisi na Udhamini Tanzania. Wakala
unatafuta Watanzania wenye sifa kujaza nafasi zifuatazo;
2.1 AFISA USAJILI MSAIDIZI DARAJA LA II – NAFASI 3
2.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusajili Ndoa, Vizazi na Vifo na Muungano wa Wadhamini na kutunza
kumbukumbu zake.
ii. Kukusanya ada za Ndoa, Vizazi na Vifo na Muungano wa Wadhamini.
iii. Kutayarisha Fahirisi (Index) za Ndoa, Vizazi na Vifo kwa wilaya na mikoa.
iv. Kutayarisha matangazo yahusuyo shughuli za mirathi yanayotolewa katika gazeti
la Serikali na hati za malipo mbalimbali kuhusu mirathi.
v. Kutunza magazeti ya Serikali, nyongeza za Sheria (Acts Supplements).
vi. Kutunza Ratiba za kesi za Mahakamani zinazohusu mirathi (Court Diary) na
kuwakumbusha Mawakili wa Serikali wanaohusika.
vii. Kupokea taarifa na kufanya upekuzi.
viii. Kuwaelekeza wananchi kuhusu utaratibu wa kuendesha mirathi.
2.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye stashahada ya Sheria (Diploma in Law).
2.1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita vilivyothibitishwa (Certified Copies) kwa wale
waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia
sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 11 Aprili, 2018.
xii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa
Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya
Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment
Portal’)
MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA
KAZI ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU
VILIVYOTHIBISHWA (CERTFIED). BARUA HIYO IELEKEZWE KWA
KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI
WA UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO