Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2018

FARAGHA YA MAOMBI

Lengo : : Kukutana na Mungu na Utukufu wake Na: Mch.John Mkuwa kutoka FPCT KISEKE Mwanadamu anahitaji kukutana na Mungu pamoja na utukufu wake.Yako maeneo mengi ambayo Mungu huweza kukutana na watu wake, baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na eneo la faragha .Kuna faragha nyingi katika maisha ya wokovu baadhi ya faragha hizo ni :- a)      Faragha ya maombi b)      Faragha ya kusoma neno c)       Faragha ya ukimya au utulivu Kama nilivyoeleza hapo juu kwamba kuna faragha nyingi leo tutaangalia faragha ya maombi.   Nini maana ya faragha ya maombi ?   Maombi ni mazungumzo ya mtu na Mungu wake.Maombi ya faragha ni mazungumzo ya mtu na Mungu katika eneo la utulivu wa akili,ukimya,upekee usio na mwingiliano wa kitu chochote.Maombi ya faragha ni maombi yenye uwezo mkubwa wa kumshusha Mungu ndiyo maana maombi haya yanatakiwa kufanyika mahali pa SIRI. SIRI YA FARAGHA   Yesu mara nyingi alifanya ...

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOOMBEA MAHITAJ

  Shalom wana wana wa Mungu !Tuna kila sababu ya kujua kwa nini hatupokei majibu ya mahitaji .Karibu tuendelee na somo letu lenye kichwa MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOOMBEA MAHITAJI.Kama hukushiriki katika sehemu ya kwanza bonyeza link hii ili usome sehemu ya kwanza. https://nsanacz.blogspot.com/2018/04/mambo-ya-kuzingatia-unapoombea-mahitaji.html SEHEMU YA PILI : VIZUIZI VINAVYOFANYA USIPATE MAJIBU KWA KIWANGO CHA JUU Yoh 14:12 a)     Kutaka miujiza tu na ukawa hutaki kumfuata Yesu katika mambo yote.(Math 6:33,Yoh 6:24-27,Zab 91:14-16) b)    Kukataa kuwa chini ya mamlaka ya Mungu.Yoh 14:31,Kumb 4:2 c)     Kutafuta kuwapendeza wanadamu badala ya Mungu.Yoh 8:29,Zab 73:25 d)    Kuigeukia miungu mingine –Kumb 31:18 e)     Viungo vyako kutumika kutenda dhambi Isa 1:15,Ez 39:24,Isa 59:2-3 f)      Kutokuwa tayari kujifunza Neno la Mungu na kulitenda –Mith 11:28,Yoh 8:29,31 g)  ...

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOOMBEA MAHITAJI

1.    Mfahamu Mungu –Ebr 11:6 a)     Anajishughulisha sana na mambo yetu -1Pet 5 :6-7 b)    Ni mapenzi yake upokee majibu ya mahitaji yako. Zab 37 :4,Yoh 16 : 24 c)     Ana huruma kwa wana wake wamchao Zab 103: 13,Luka 7: 13-15 d)    Mungu hana tabia ya kusahau,hawaachi,hawapungukii wala hawatupi watoto     watoto wake Zab 94 :14,Kumb 31:8. Ukisoma maandiko andiko Isaya 16 Tazama, nimekuchora katika viganga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima. Daudi anasema nalikuwa ni kijana na sasa ni mzee Zab 37 :25,28).Isa 12:21,1falm 6:13 e)     Ni mzaliwa wa kwanza Ebr 2 :11,Rum 8 :29 2.     Fahamu ulivyo wa thamani mbele za Mungu. a.     Wewe ni taji ya uzuri mbele za Mungu Isa 62:3 b.     Wewe ni mboni ya jicho la Mungu Zek 2:8 c.     Wewe ni kito au jiwe la thamani linalometa meta Zek 9 :16 d.  ...

WOKOVU NI KUWA NA USHIRIKA

 Sehemu ya pili   K WELI KUU: Maisha yetu ya wokovu hayana maana kabisa kama hatutakuwa na ushirika na Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na sisi kwa sisi kama kanisa la Kristo ambalo ni mwili wa Kristo. ​ Mstari wa Msingi (Kukumbuka): 1 Wakorintho 1:9 Mungu ni mwamainifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe , Yesu Kristo Bwana wetu. ​ UTANGULIZI Katika utangulizi, sehemu ya kwanza ya somo letu tuliangalia maana ya “ ushirika ” na maana ya “ uhusiano au mahusiano ” na pia tulipata kubainisha na kuainisha kwa kifupi sana viini (essences) vya ushirika. Leo katika utangulizi wetu nataka twende mbele kidogo kwa kuangalia ni nini maana ya “wokovu”; usisahau somo letu ni “ Wokovu Ni Kuwa Na Ushirika ” na bado tupo kwenye utangulizi ambapo tunaangalia maana ya maneno muhimu; wokovu, uhusiano na ushirika. WOKOVU MAANA YAKE NINI? Wokovu ni ukombozi wa mwanadamu kutoka katika vifungo vyote vya mauti na kuzimu kwa ...