FARAGHA YA MAOMBI
Lengo : : Kukutana na Mungu na Utukufu wake
Na: Mch.John Mkuwa kutoka FPCT KISEKE
Mwanadamu anahitaji
kukutana na Mungu pamoja na utukufu wake.Yako maeneo mengi ambayo Mungu huweza
kukutana na watu wake, baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na eneo la faragha .Kuna
faragha nyingi katika maisha ya wokovu baadhi ya faragha hizo ni :-
a) Faragha ya maombi
b) Faragha ya kusoma neno
c) Faragha ya ukimya au
utulivu
Kama nilivyoeleza hapo juu
kwamba kuna faragha nyingi leo tutaangalia faragha ya maombi.
Nini maana ya faragha ya maombi ?
Maombi ni mazungumzo ya mtu
na Mungu wake.Maombi ya faragha ni mazungumzo ya mtu na Mungu katika eneo la
utulivu wa akili,ukimya,upekee usio na mwingiliano wa kitu chochote.Maombi ya
faragha ni maombi yenye uwezo mkubwa wa kumshusha Mungu ndiyo maana maombi haya
yanatakiwa kufanyika mahali pa SIRI.
SIRI YA FARAGHA
- Yesu mara nyingi alifanya maombi ya faragha
- Mikataba mikubwa ya Nchi hufanyika mahali pa faragha
- Mazungumzo yenye maana na nguvu hufanyika mahali pa faragha
- Mfalme herode aliwaita Mama jusi mahali pa faragha.
- Mambo mazito na ya siri huzungumzwa faragha.
Faragha ni muhimu sana kwa
maisha ya :-
a)
Huduma
Watumishi wanakuwa busy na
huduma kuliko kuwa busy na mtoa huduma.Huduma ya kuhubiri neno la Mungu na
kuwahudumia watu wa MUNGU inahitaji muda mwingi mtumishi awe na tabia ya kuwa
na faragha na Mungu.
b)
Ndoa
Ndoa nyingi zina migogoro
na zimeingia katika migogoro kwa sababu hakuna faragha kati ya wanandoa kila
kitu hufanywa hadharani.
c)
Maisha ya familia.
Watoto wengi wanaharibika
kwa sababu hawana faragha au walikosa faragha kutoka kwa wazazi wao.Wazazi
wanachukulia kuwa watoto hawana mchango wowote katika maamuzi ya kifamilia na
hivyo hakuna muda wa kuwasikiliza kile wanachofikiria.
d)
Maisha ya kazi na biashara
Kila kazi inahitaji faragha
ili akili iumbike upya .Ndiyo maana hata wachungaji wanahitaji kuwa na likizo
ili akili iumbike upya.Wafanyakazi wa Serikali na sekta wanapata likizo
ulishajiuliza kwa nini hivyo ?.Wafanyabiashara wanakuwa na muda wa kufurahia
kazi na kutafakari biashara kwa kwenda sehemu zenye vivutio ili kubadili mifumo
ya ufanyaji biashara.
“Basi wale mitume
waliporudi walimweleza mambo yote waliyoyatenda ; akawachukua ,akaenda nao
faraghani mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida”Luka 9: 10 Ukiangalia kwa kina
utagundua kuwa Yesu alithamini kukutana na wanafunzi wake mahali pa Siri ili
kutatua changamoto zao nap engine kufanya maandalizi ya kazi kubwa na uponyaji
wa watu.
Dr.MYLES MUNROE anasema“If
you spent four hours in the morning with God you will use a minute to solve
human problems” Tafsiri isiyo rasmi ni ukitumia masaa manne na Mungu
kabla ya kupambazuka utatumia muda mchache kumaliza matatizo ya watu”
Akawaambia ,njoni peke yenu
kwa faragha ,mahali pasipokuwa na watu,mkapumzike kidogo.Kwa sababu walikuwako
watu wengi,wakija ,wakienda ,hata haikuwapo nafasi ya kula.Marko 6:31
Soma pia mathayo 24:1-3
……………… hata alipokuwa
ameketi katika mlima wa mizeituni,wanafunzi wake walimwendea kwa faragha…………………….
Ø
Tujifunze kutatua mambo yetu mahali pa faragha.
Ø
Jifunze kusoma watu na hali zao,ukiona huwezi kufanya mazungumzo nao
hadharani waite faraghani.
Ø
Kukosekana kwa faragha kuna ua huduma
Ø
Usiwe busy na huduma uwe busy na mtoa huduma
Ø
Yesu pamoja na uwezo wote alithamini kuwa na faragha sana,mara utasikia
akisema na tuvuke ng’ambo.Lakini pia alitumia miaka mitatu kufanya huduma hapa
duniani baadae akaondoka.Lakini watumishi wanashika madhabahu kila siku,kila
wiki,kila mwezi ,kila mwaka na miaka yote.Hapana hii lazima italeta shida
katika utumishi wako .Jitafakari ?,Chukueni likizo hata mwezi mwende kupumzika.
Soma Math 14:13,22-23.17:1-8
Mwisho :
ü
Tunahitaji kufanya maombi ya faragha,mahali ambapo simu imezimwa hakuna
mwingiliano wa kitu chochote.
ü
Unachelewa kukutana na MUNGU kwa kuwa huna faragha naye.Mungu anatabia
yakukutana na watu faraghani.
ü
Ni afadhali kulala kanisani kwenye mkesha maombi peke yako,
ü
Tumia muda ambao hakuna watu kanisani uende wewe ukutane na Mungu.
ü
Mungu aliyekutana na Mungu faragha huwezi kumbabaisha na wala hawezi
kukutemeshwa na chochote.\
Barikiwa sana.
Somo hili lilifundishwa na
Mchungaji John Mkuwa FPCT KISESA 08APRIL 2018
Maoni