KUSIMAMISHA MISINGI YA UFALME WA MUNGU ILI UINULIWE
Na.AYOUB J.LEO
FPCT KISESA,MWANZA
UTANGULIZI
Zab
11 :3 “Kama misingi ikiharibika mwenye haki atafanyaje ?
VIPENGELE
MUHIMU KATIKA SOMO HILI.
1.  
TAMBUA
UWEPO WA MISINGI
Kila
jambo lina msingi wake katika maisha.
a)    Msingi
wa maisha ya Kiroho ni utawala wa Mungu (Nuru) ;Zab 89:11,Isa 60:1
b)   Msingi
wa Imani yetu umejengwa juu ya YESU KUHANI MKUU; Ef 2:18-22,
c)    Msingi
wa Yerusalemu mpya-Umejengwa juu ya makabila 12 ya Israeli ( Uf
21:14,19-21,Kumb 33:1( Mawe 12 ni tabia za wana wa
YAKOBO)Unyenyekevu,usikivu,utoaji,uaminifu,imani,upendo,uvumilivu,msamaha,umoja,moyo
wa toba,upatanishi na maombi).
2.    JE MISINGI INAWEZA KUHARIBIKA ? Jibu
ni ndiyo misingi inaweza kuharibiwa ,ndiyo maana andiko linaeleza kama misingi
ikiharibika hivyo tunapaswa kujua kuwa upo uwezekano wa kuharibu misingi.
3.  
 NINI
HUTOKEA MISINGI IKIHARIBIKA ?
a)    Uharibifu
wa kila namna hutokea; Ezek 22:23-29
b)   Waaminifu
hutoweka (hukosekana) –Zab 12 :1-2
c)    Gadhabu
ya Mungu huachiliwa –Ez 22:30-31
     4.  MISINGI IKIHARIBIKA MWENYE HAKI AFANYE NINI ?
Isa 24:20
        Zab 11 :3 “Kama misingi ikiharibika
mwenye haki atafanyaje ?
§  Maandiko
yanapouliza nini mwana wa Mungu akifanye ikiwa misingi imeharibiwa ujue upo
uwezekano wa kuisimamisha misingi iliyoharibika ? Ezek 22:3031,Yer 5:1-5,Tafakari
Eze 2:1
a)    Fanya
matengenezo ( Toba ya kweli) Yer 3:13,Isa 1:16-17,Ezra 10:11,
b)   Mkabidhi
Mungu Ebr 6:1
ü  Mungu
akikabidhiwa anatikisa na kufungua milango Mdo 16:25-26
ü  Ataweka
msingi wake  1cor 3:10,Zab 87 :1,89:3-4
ü  Msingi
wake ni imara 2 Tim 2:19-22
ü  Msingi
wake ni mzuri ( umepambwa) Isa 54:11-12
ü  Msingi  wake unawapa amani nyingi watoto wako Isa
54:13
     c) Mwinue Yesu  (Yoh 3: 14,8:28.). 
         Yesu akiinuliwa juu,yeye    anakuvuta 
Yoh 12:32,3:14,Hes 21: 4-9
      5. 
NAMNA YA KUSIMAMISHA MISINGI
ü   Fanya toba ya kweli. Watumishi waliotangulia
walifanya toba mara baada ya kugundua kilichowapata.
·        
Toba ya Daudi   Zab 51:1-19
·        
Toba ya Daniel  Dan 9:4- 19,Matokeo yake Dan 9:20-23
·        
Toba ya Ezra na Nehemia
ü  Bomoa
misingi yote isiyotokana na Mungu Yer 1: 10, 51 :20-23, Kata kitovu
kinachokuletea madhara (Ezek 16 : 4 )
ü  Rejesha
misingi yote iliyojengwa na Mungu.
·        
Musa alirejea kwenye msingi    (Kut 24:4 )
·        
Eliya alirejea kwenye Msingi  ( 1fal 18 :30 -31)
·        
Yesu alirejesha msingi ulioharibiwa
na Adam ( Rum 5: 12 – 14),Yeye akateua mitume 12,akaweka msingi mpya
usioshindwa na milango ya kuzimu. Math 16 :18.
Watakatifu
wamejengwa juu ya YESU 1Pet 2 :5,1 Cor 3 : 9-14.
ü  Amini
kuwa kuna uwezekano wa kuinuka         Zab
113: 7
Maoni