KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
KARAMA ZA UWEZO i) Karama ya Imani Awali ya yote, kabla sijaichambua karama ya imani, hebu nitoe tafsiri fupi ya msamiati wa neno imani kibiblia ina maana gani. Imani ni “hisia ya rohoni za kuwa na hakika na mambo ya ki-Mungu zikiwemo ahadi zake pamoja na kutambua uwepo wake kama Mungu Muumbaji na mwenye uwezo wote,asiyeshindwa lo lote na yuko mahali pote na anajua mambo yote. Kitabu cha Waebrania kimeandika kwamba: “Basi, imani ni KUWA na hakika ya mambo yatarajiwayo, na bayana ya mambo yasiyoonekana bado.” (EBR 11:1) Imani hii chanzo chake ni Injili ya wokovu inapohubiriwa kwa mwenye dhambi, akaisikia ndipo hushawishika na kuanza KUWA na hakika ya ukombozi wa Yesu Kristo. Kitabu cha Warumi kimeandika chimbuko la Imani kuwa: “chanzo cha imani ni kusikia, na kusikia kunatokana na Neno la Kristo.” (Rum.10:17) Kila mwamini aliyeokoka anayo imani ya Kristo. Kwa imani hiyo, amepokea wokovu na kuhes...