SHUKRANI. Ninamshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kukufikia mtu wa Mungu kupitia ujumbe huu. Pia ninamshukuru mke wangu mpendwa Jane Ayoub kwa kunitia hamasa ya kufanya kazi ya Mungu.Pia watoto wangu Bernadetha Ayoub,Bertha Ayoub na Bernice Ayoub,kwa kuniombea na kuvumilia upweke wangu kwao. Siwezi kusahau watumishi wa Mungu walioandika na kufundisha masomo yanayofanana na somo hili.Nimejifunza mambo mazuri yaliyofanyika msaada kwangu.Nitataja wachache 1. Dr.Myles Munroe 2. Pastor Chris Oyakilome (PHD) 3. Dr.Mensa Otabil 4. Rev.Primus Muabuzi 5. Mwl, Christopher Mwakasege 6. Bishop Augustine Mpemba 7. Mch.John Mkuwa 8. Fredrick Eliakim 9. July Bosha- Kiongozi na mlezi wangu Kiroho Ninakushauri unaposoma kijitabu hiki utulie kwa makini na kutafakari kwa kina.Nukuu zimetoka katika maandiko matakatifu yaani Biblia.Mahali pengine nimenukuu maandiko ya semina na mafundisho kutoka kwa wapakwa Mafuta wa Bwana.Nina imani utabarikiwa.Ayoub
Na, Rev. Innocent Kamote SEHEMU YA 1: KITABU CHA DANIELI. SOMO LA 1: KUPITIA YA KITABU CHA DANIELI : A; D A N I E L I: Lengo la 1; - Eleza Historia fupi ya Danieli. Danieli – jina lake lina maana “ Mungu ndiye Hakimu wangu ”. Alikuwa mmojawapo wa mateka waliochukuliwa na mfalme Nebukadneza katika mwaka 605 KK. Kutoka Yerusalemu na kupelekwa Babeli. Aliishi kipindi chote cha utumwa cha miaka 70 huku akiwa nabii na mwandishi wa Kitabu cha Danieli. Tunamfahamu Danieli jinsi alivyokuwa mcha Mungu, tukisoma Eze.14:14-20. Inavyoonekana alitokea na ukoo wa daraja la juu huko Yerusalemu. Danieli hakuwahi kuoa, inawezekana alifanywa towashi kwa sababu alifanya Kazi katika Kasri la mfalme. B. KITABU CHA DANIELI: Lengo la 2 : Taja tarehe na makusudi ya kuandikwa kitabu hiki. Kitabu hiki kiliandikwa kati ya mwaka 536 – 530 KK. Kikiwa na m
SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO Na Ayoub Jacob Leo,FPCT KISESA 13.11.2016 hadi 27.11.2016 Nini maana ya Agano? Maana: Ni mapatano au makubaliano yanayowekwa baina ya pande mbili au zaidi ili kutekeleza jambo/mkakati uliopo.Katika Maandiko kuna maagano mengi yaliyowekwa na Mungu na watu au watumishi wake. Mfano Agano la Mungu na Adam Edeni,Mungu na Nuhu,Mungu na Ibrahim,Mungu na Musa,Agano la kanisa la leo kwa damu ya Yesu( Math 26:28) MSINGI WA AGANO LA DAMU YA YESU Yer 31:31-33,Ebr 8:8 · Agano hilo linatambulishwa kuwa jipya · Halitafanana na agano lolote lile · Agano litatia sheria ndani ya mioyo yao. · Ndani ya mioyo yao zitaandikwa · Agano litawafanya watu wa Mungu kuwa milki yake. Damu ya Yesu ina nguvu kupita agano lolote :- ( Math 26:28a) · Damu ya Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi Math 26 :28,1Yoh 1:7-8 “ Na kila Kuhani husimama kila siku akifanya ibada,
Maoni