Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2018
NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
SEHEMU YA NNE B Na: Patrick Sanga Nafasi ya tano – Mwanamke kama Mjenzi Katika sehemu ya 4a tulianza kwa kuangalia nafasi ya tano hata hivyo kutokana na urefu wake nikaona vema kuigawanya nafasi hii ya tano katika kipengelea a na b. Ili kusoma sehemu ya 4a bonyeza link ifuatayo https://nsanacz.blogspot.com/2018/05/namna-mwanamke-anavyoweza-kutumia_47.html Katika sehemu ya 4b tutangalia ni kwa namna gani mwanamke atapata hekima ya kumsaidia kujenga ndoa yake. Karibu sasa tuendelee… Hebu tuanze kwa kuangalia mstari wa ajabu sana katika Muhubiri 7: 12 unasema ‘Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi, na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliyonayo’ . Hekima ndio nguzo kuu ya ujenzi wa ndoa yako, naam ukiwa nayo ni dhahiri kwamba italeta uponyaji kwenye ndoa yako pia. Mwanamke kama mjenzi anahitaji kuwa na hekima ili kulinda ndoa yake akijua kwamba ki – nafasi yeye ni Mlinzi wa mumewe. Kumbuka kwamba andiko letu la msingi katika sehemu
NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE (Sehemu ya 4a)
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Na: Patrick Sanga Nafasi ya tano – Mwanamke kama Mjenzi Katika sehemu ya tatu tuliangalia nafasi ya nne ambayo ni Mwanamke kama Mlinzi. Ili kuisoma endapo hukusoma bonyeza link hii https://nsanacz.blogspot.com/2018/05/namna-mwanamke-anavyoweza-kutumia_6.html. Fuatana nami sasa tuendelee na mfululizo wa somo hili. Biblia katika kitabu cha Mithali 14:1 inasema ‘ Kila mwanamke aliye na hekima huijenga nyumba yake: Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’. Tafsiri ya neno nyumba ni familia, naam na familia inajumuisha baba, mama na watoto endapo mmejaliwa. Hata hivyo katika hali ya kawaida watoto watalelewa katika msingi mzuri endapo ndoa husika imetengamaa. Ifahamike kwamba hili andiko si la wanandoa peke yao, bali hata wanawake wasio wanandoa wenye familia kama wajane, walezi nk linawahusu. Kwa kuwa hapa tunazungumzia habari za wanandoa nitalifafanua zaidi kutoka kwenye kona hiyo. Pia neno nyumba limetumika ili kutupatia urahisi wa kuelewa namna nyumba
NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE (Sehemu ya 3)
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Na: Patrick Sanga Nafasi ya nne – Mwanamke kama Mlinzi Katika sehemu ya pili tuliangalia nafasi tatu za awali ambazo ni nafasi ya Msaidizi, Mshauri na Mleta kibali . Ili kusoma sehemu ya pili bonyeza link hii https://nsanacz.blogspot.com/2018/05/namna-mwanamke-anavyoweza-kutumia_4.html .Kumbuka kwamba lengo la ujumbe ni kuangalia ni kwa namna gani Mwanamke aliyeolewa anaweza kutumia nafasi zake kubadilisha/kuiponya ndoa yake. Katika sehemu hii ya tatu tutaangalia nafasi ya mwanamke kama Mlinzi. Naam kwa rejea kumbuka kwamba, msingi wa somo hili ni maneno ambayo Octoba 2009 BWANA aliniambia akisema ‘ Waambie wanawake wasimame kwenye nafasi zao ndipo wataona uponyaji kwenye ndoa zao’ . Labda nianze kwa kuuliza, je una fahamu kwamba wajibu wa kumlinda mumeo ni wako? Naam Mungu amejiwekea utaratibu mpya kwamba Mwanamke amlinde mwanaume. Je ni ulinzi wa namna gani? Ni ulinzi wa kiroho ndio ambao mwanaume anahitaji kutoka kwa mkewe. Mke anatakiwa kuwa makini ‘sensiti
NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE (Part 2)
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Na: Patrick Sanga Maada: Nafasi ya Msaidizi, Mshauri na Mleta kibali Ili kusoma sehemu ya kwanza bonyeza link hii https://nsanacz.blogspot.com/2018/05/namna-mwanamke-anavyoweza-kutumia.html Mpenzi msomaji, Mungu akubariki kwa kufuatilia mfululizo wa somo hili. Ni imani na maombi yangu kwamba masomo haya yatafanyika msaada kwenye maisha yako na ndoa yako kwa ujumla. Katika sehemu hii ya pili nitaandika kuhusu nafasi tatu ambazo ni nafasi ya Mwanamke kama Msaidizi, Mshauri na Mleta kibali. Mwanamke kama Msaidizi Mwanzo 2:18 ‘ BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye’ . Ukisoma mstari huu katika toleo la GNB Biblia inasema ‘ Then the LORD God said, “It is not good for the man to live alone. I will make a suitable companion to help him. ” Biblia inatueleza kwamba Adam ndiye aliyetangulia kwanza kudhihirishwa kabla ya Mwanamke. Kabla ya Hawa kuletwa, Mungu alimpa Adam majukumu mengi ambayo alipaswa kuyatekel
NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Na: Patrick Sanga Mithali 14: 1 ‘Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’ . Mchungaji mmoja rafiki yangu aliniambia asilimia hamsini mpaka sabini ya changamoto au matatizo anayoshughulika nayo mara kwa mara katika kanisa lake ni ya wanandoa. Kwa lugha nyepesi asilimia 50 – 70 ni matatizo yatokanayo au yanayohusiana na ndoa. Binafsi pia kwa upande wangu kupitia nafasi yangu katika mwili wa Kristo, email za wasomaji ninazopata na pia baadhi ya semina za ndoa ambazo nimefanya kuhusu eneo hili nimegundua kwa hakika ndoa nyingi za wana wa Mungu zina shida na wao hawajajua kwamba vita hii inatoka kwa Shetani, maana anajua ndoa zikitengamaa ni faida kwa ufalme wa Mungu na ni uharibifu kwenye ufalme wake wa giza. Naam anapigana usiku na mchana ili kuhakikisha ndoa hazitengamai kwa kuleta fujo za kila aina. Kila siku katika ndoa kuna changamoto zinazaliwa mpaka imefika mahala baadhi ya wanandoa wanawaza kwa