Machapisho

WOKOVU NI KUWA NA USHIRIKA

 Sehemu ya pili   K WELI KUU: Maisha yetu ya wokovu hayana maana kabisa kama hatutakuwa na ushirika na Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na sisi kwa sisi kama kanisa la Kristo ambalo ni mwili wa Kristo. ​ Mstari wa Msingi (Kukumbuka): 1 Wakorintho 1:9 Mungu ni mwamainifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe , Yesu Kristo Bwana wetu. ​ UTANGULIZI Katika utangulizi, sehemu ya kwanza ya somo letu tuliangalia maana ya “ ushirika ” na maana ya “ uhusiano au mahusiano ” na pia tulipata kubainisha na kuainisha kwa kifupi sana viini (essences) vya ushirika. Leo katika utangulizi wetu nataka twende mbele kidogo kwa kuangalia ni nini maana ya “wokovu”; usisahau somo letu ni “ Wokovu Ni Kuwa Na Ushirika ” na bado tupo kwenye utangulizi ambapo tunaangalia maana ya maneno muhimu; wokovu, uhusiano na ushirika. WOKOVU MAANA YAKE NINI? Wokovu ni ukombozi wa mwanadamu kutoka katika vifungo vyote vya mauti na kuzimu kwa ...

WOKOVU NI KUWA NA USHIRIKA

SEHEMU YA KWANZA KWELI KUU: Maisha yetu ya wokovu hayana maana kabisa kama hatutakuwa na ushirika na Baba, Mwana, Roho Mtakatifu, na sisi kwa sisi kama kanisa la Kristo ambalo ni mwili wa Kristo. ​ Mstari wa Msingi (Kukumbuka): 1 Wakorintho 1:9 Mungu ni mwamainifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe , Yesu Kristo Bwana wetu. ​ Ndugu mpendwa, leo nitaanza mfululizo wa somo hili ambalo litakuwezesha wewe kueneza mizizi yako ya imani katika Yesu Kristo Bwana wetu ambaye ni Mungu Mwana, na katika Mungu Roho Mtakatifu na katika Mungu Baba kwa kujua nini maana ya kuwa na ushirika, namna ya kuwa na ushirikana jinsi ya kuendelea kuwa na ushirika Mungu (Baba, Mwana na Roho Matakatifu). Karibu sana. UTANGULIZI: Katika utangulizi wetu, tutaangalia zaidi maana ya maneno makuu matatu ambayo yatajitokeza katika somo letu hili na miongoni mwa maneno hayo mawili yamejitokeza katika kichwa cha somo letu. Hivyo ni lazima tuyaangalie ili tuwe na ...

KUSIMAMISHA MISINGI YA UFALME WA MUNGU ILI UINULIWE

Na.AYOUB J.LEO FPCT KISESA,MWANZA UTANGULIZI Zab 11 :3 “Kama misingi ikiharibika mwenye haki atafanyaje ? VIPENGELE MUHIMU KATIKA SOMO HILI. 1.    TAMBUA UWEPO WA MISINGI Kila jambo lina msingi wake katika maisha. a)     Msingi wa maisha ya Kiroho ni utawala wa Mungu (Nuru) ;Zab 89:11,Isa 60:1 b)    Msingi wa Imani yetu umejengwa juu ya YESU KUHANI MKUU; Ef 2:18-22, c)     Msingi wa Yerusalemu mpya-Umejengwa juu ya makabila 12 ya Israeli ( Uf 21:14,19-21,Kumb 33:1( Mawe 12 ni tabia za wana wa YAKOBO)Unyenyekevu,usikivu,utoaji,uaminifu,imani,upendo,uvumilivu,msamaha,umoja,moyo wa toba,upatanishi na maombi). 2.     JE MISINGI INAWEZA KUHARIBIKA ? Jibu ni ndiyo misingi inaweza kuharibiwa ,ndiyo maana andiko linaeleza kama misingi ikiharibika hivyo tunapaswa kujua kuwa upo uwezekano wa kuharibu misingi. 3.      NINI HUTOKEA MISINGI IKIHARIBIKA ? a)     Uharibifu wa k...

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

Na, Rev. Innocent Kamote        SEHEMU YA 1:   KITABU CHA DANIELI.                                            SOMO LA 1:   KUPITIA   YA KITABU CHA DANIELI : A;             D A N I E L I:                 Lengo la 1;   - Eleza Historia fupi ya Danieli. Danieli – jina lake lina maana “ Mungu ndiye Hakimu wangu ”.   Alikuwa mmojawapo wa mateka waliochukuliwa na mfalme Nebukadneza katika mwaka 605 KK. Kutoka Yerusalemu na kupelekwa Babeli.   Aliishi kipindi chote cha utumwa cha miaka 70 huku akiwa nabii na mwandishi wa Kitabu cha Danieli.   Tunamfahamu Danieli jinsi alivyokuwa mcha Mungu, tu...