Machapisho

NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE (Part 2)

Picha
Na: Patrick Sanga Maada: Nafasi ya Msaidizi, Mshauri na Mleta kibali   Ili kusoma sehemu ya kwanza bonyeza link hii https://nsanacz.blogspot.com/2018/05/namna-mwanamke-anavyoweza-kutumia.html Mpenzi msomaji, Mungu akubariki kwa kufuatilia mfululizo wa somo hili. Ni imani na maombi yangu kwamba masomo haya yatafanyika msaada kwenye maisha yako na ndoa yako kwa ujumla. Katika sehemu hii ya pili nitaandika kuhusu nafasi tatu ambazo ni nafasi ya Mwanamke kama Msaidizi, Mshauri na Mleta kibali. Mwanamke kama Msaidizi Mwanzo 2:18 ‘ BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye’ .  Ukisoma mstari huu katika toleo la GNB Biblia inasema ‘ Then the LORD God said, “It is not good for the man to live alone. I will make a suitable companion to help him. ” Biblia inatueleza kwamba Adam ndiye aliyetangulia kwanza kudhihirishwa kabla ya Mwanamke. Kabla ya Hawa kuletwa, Mungu alimpa Adam majukumu mengi ambayo alip...

NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE

Picha
Na: Patrick Sanga Mithali 14: 1 ‘Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’ . Mchungaji mmoja rafiki yangu aliniambia asilimia hamsini mpaka sabini ya changamoto au matatizo anayoshughulika nayo mara kwa mara katika kanisa lake ni ya wanandoa. Kwa lugha nyepesi asilimia 50 – 70 ni matatizo yatokanayo au yanayohusiana na ndoa. Binafsi pia kwa upande wangu kupitia nafasi yangu katika mwili wa Kristo, email za wasomaji ninazopata na pia baadhi ya semina za ndoa ambazo nimefanya kuhusu eneo hili nimegundua kwa hakika ndoa nyingi za wana wa Mungu zina shida na wao hawajajua kwamba vita hii inatoka kwa Shetani, maana anajua ndoa zikitengamaa ni faida kwa ufalme wa Mungu na ni uharibifu kwenye ufalme wake wa giza. Naam anapigana usiku na mchana ili kuhakikisha ndoa hazitengamai kwa kuleta fujo za kila aina. Kila siku katika ndoa kuna changamoto zinazaliwa mpaka imefika mahala baadhi ya wanandoa wanawaza kwa ...

FARAGHA YA MAOMBI

Lengo : : Kukutana na Mungu na Utukufu wake Na: Mch.John Mkuwa kutoka FPCT KISEKE Mwanadamu anahitaji kukutana na Mungu pamoja na utukufu wake.Yako maeneo mengi ambayo Mungu huweza kukutana na watu wake, baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na eneo la faragha .Kuna faragha nyingi katika maisha ya wokovu baadhi ya faragha hizo ni :- a)      Faragha ya maombi b)      Faragha ya kusoma neno c)       Faragha ya ukimya au utulivu Kama nilivyoeleza hapo juu kwamba kuna faragha nyingi leo tutaangalia faragha ya maombi.   Nini maana ya faragha ya maombi ?   Maombi ni mazungumzo ya mtu na Mungu wake.Maombi ya faragha ni mazungumzo ya mtu na Mungu katika eneo la utulivu wa akili,ukimya,upekee usio na mwingiliano wa kitu chochote.Maombi ya faragha ni maombi yenye uwezo mkubwa wa kumshusha Mungu ndiyo maana maombi haya yanatakiwa kufanyika mahali pa SIRI. SIRI YA FARAGHA   Yesu mara nyingi alifanya ...

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOOMBEA MAHITAJ

  Shalom wana wana wa Mungu !Tuna kila sababu ya kujua kwa nini hatupokei majibu ya mahitaji .Karibu tuendelee na somo letu lenye kichwa MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOOMBEA MAHITAJI.Kama hukushiriki katika sehemu ya kwanza bonyeza link hii ili usome sehemu ya kwanza. https://nsanacz.blogspot.com/2018/04/mambo-ya-kuzingatia-unapoombea-mahitaji.html SEHEMU YA PILI : VIZUIZI VINAVYOFANYA USIPATE MAJIBU KWA KIWANGO CHA JUU Yoh 14:12 a)     Kutaka miujiza tu na ukawa hutaki kumfuata Yesu katika mambo yote.(Math 6:33,Yoh 6:24-27,Zab 91:14-16) b)    Kukataa kuwa chini ya mamlaka ya Mungu.Yoh 14:31,Kumb 4:2 c)     Kutafuta kuwapendeza wanadamu badala ya Mungu.Yoh 8:29,Zab 73:25 d)    Kuigeukia miungu mingine –Kumb 31:18 e)     Viungo vyako kutumika kutenda dhambi Isa 1:15,Ez 39:24,Isa 59:2-3 f)      Kutokuwa tayari kujifunza Neno la Mungu na kulitenda –Mith 11:28,Yoh 8:29,31 g)  ...

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOOMBEA MAHITAJI

1.    Mfahamu Mungu –Ebr 11:6 a)     Anajishughulisha sana na mambo yetu -1Pet 5 :6-7 b)    Ni mapenzi yake upokee majibu ya mahitaji yako. Zab 37 :4,Yoh 16 : 24 c)     Ana huruma kwa wana wake wamchao Zab 103: 13,Luka 7: 13-15 d)    Mungu hana tabia ya kusahau,hawaachi,hawapungukii wala hawatupi watoto     watoto wake Zab 94 :14,Kumb 31:8. Ukisoma maandiko andiko Isaya 16 Tazama, nimekuchora katika viganga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima. Daudi anasema nalikuwa ni kijana na sasa ni mzee Zab 37 :25,28).Isa 12:21,1falm 6:13 e)     Ni mzaliwa wa kwanza Ebr 2 :11,Rum 8 :29 2.     Fahamu ulivyo wa thamani mbele za Mungu. a.     Wewe ni taji ya uzuri mbele za Mungu Isa 62:3 b.     Wewe ni mboni ya jicho la Mungu Zek 2:8 c.     Wewe ni kito au jiwe la thamani linalometa meta Zek 9 :16 d.  ...